Monday 15 July 2013

COASTAL B NA AZAM B WALIVYOUGEUZA UWANJA WA SOKA KUWA ULINGO WA MIELEKA NA NDONDI

Mchezo wa Azam B dhidi ya Coastal union B ya Tanga umemalizika kwa kuzusha vurugu na kusababisha mchezaji mmoja wa Azam kujeruhiwa vibaya.
Habari zilizotufikia kutoka jijini Arusha  timu hizo zilipokuwa zikishiriki michuano ya Rolling Stone inayoandaliwa na kituo hicho cha kulelea vijana wenye vipaji inasema vurugu hizo zililizuka mara baada ya wachezaji wa timu ya Azam B kwenda kuwazomea Coastal Union B katika basi lao
baada ya kuwafunga na kuwatoa kwa mikwaju ya penati 5-4.
Katika mchezo huo mchezaji wa Azam alipigwa na chuma na kujeruhiwa vibaya na mchezaji mwenzake wa Coastal Union.
Fainali ya Rolling Stone itawakutanisha Azam Academy dhidi ya Eagle Rangers Academy ya Tanga mara baada ya Eagle kuwatoa under 20 ya Oljoro kwa kuwafunga mabao 2-1.
PALIKUWA HAPATOSHI WACHEZAJI WA COASTAL UNION WAKIZUIWA NA WENZAO NA VIONGOZI NA MASHABIKI WASIENDE KUWAJERUHI WENZAO.
MCHEZAJI WA AZAM B AKIWA AMELALA CHINI MARA BAADA YA KUJERUHIWA KATIKA VURUGU HIZO
VIONGOZI WA AZAM FC WAKIJADILIANA JAMBO KATIKA VURUGU HIZO
KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA FFU WAKIINGIA UWANJANI HAPO KUTULIZA VURUGU HIZO
MCHEZAJI CHUMA WA COASTAL UNION AKIZUILIWA NA WENZAKE BAADA YA KUPANDWA NA HASIRA

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako