ULE msemo wa maji hufuata mkondo ndio unaoonekana
kujidhihirisha kwa mtoto wa gwiji la zamani la soka Andy Cole aliyewahi
kukipiga Manchester City lakini akitamba sana na Manchester United baada ya
kinda la nguli huyo linalojulikana kwa jina la
Devante Cole kujumuishwa kikosini na kocha wa
Manchester City Emanuel Pelegrin katika safari ya kujiandaa na msimu.
Devante anaecheza nafasi ya mshambuliaji wa kati
kama alivyokuwa baba yake anaonekana kurithi utaalamu na ujuzi kama aliokuwa
nao baba yake enzi hizo akisakata kabumbu.
Kikosi cha Manchester City kinatarajia kuanza michezo yake ya
kujiandaa na msimu tarehe 14 nchini Africa kusini kwa kucheza dhidi ya super
sport mjini Pretoria na pia baada ya siku nne watacheza Na Amazulu mjini Durban
 |
MTOTO WA M WANASOKA WA ZAMANI ANDY COLE AITWAYE DEVANTE COLE AKIFANYA VITU VYAKE UWANJAMNI |
ENZI YA ANDY COLE AKIKIPIGA KUNAKO CLUB YA MAN CITY
 |
MTOTO WA COLE AKIONESHA MAUTUNDU YA KUUCHEZEA MPIRA KWA ,KICHWA NA MCHEZAJI MWENZAKE NJE YA UWANJA WA MANCHESTER CITY. |
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako