Kisiwa cha Palm ni kisiwa kilichopo Dubai, United Arab
Emirates (UAE), pembezoni kwa Persian Gulf, kimebuniwa na Nakheel properties kwa
matumizi ya kibiashara pamoja na kuishi kasha kikaendelezwa kwa hisani ya UAE.
Muundo wake kama
unavyoonekana ni kama mti na kisiwa kina ukubwa wa Kilometer za mraba 520,
ambapo kuna hotel zaidi ya 100 za kufahari zenye fukwe nzuri, migahawa, maduka,
maeneo ya michezo pamoja na eneo la mazoezi.
Kisiwa hicho kimejengwa mwaka
2002 na kumalizika October 2006.
Kisiwa cha
palm kilitangazwa kwa maendeleo octoba 2004. Makadirio ya mwanzo ya muundo na
ukubwa wake yalikuwa mara nane ya ukubwa wa palm Jumeirah na mara tano ya ukubwa wa palm jebel Ali. Kisiwa cha Palm Deira kinalengwa kuwapa
makazi watu milioni moja.
Mwanzo muundo wa eneo la kisiwa ulionekana kuwa na
ukubwa wa kilometa14 kwa kilometa 8.5. kutokana na mabadiliko ya kina cha gofu
ya Persia kisiwa cha palm Deira kilibadilishwa muundo wake mwezi wa tano mwaka
2007. Mabadiliko hayo yalikua na muundo mpya wa kilometa 12.5 kwa 7.5
Mapema octoba 2007, asilimia
20 ya ardhi ya kisiwa cha Palm (millioni 200 cubic meta za ardhi) ilikua tayari
imemalizika kuandaliwa kwa shughuli mbalimbali za maendeleo na eneo hilo
lilikua linatumika rasmi.
Mwanzoni mwa mwezi wa nne 2008 Nakheel (kisiwa cha
palm) kilitangaza kwamba zaidi cubic meta millioni 300 ambayo ni robo ya eneo
la kisiwa cha palm limeshawahiwa.
Kutokana na ukubwa wa kisiwa cha
Palm kisiwa kimegawanywa katika vieneo vidogo vidogo, eneo la kwanza ni eneo la
kisiwa cha Deira. Eneo hili litakua kati ya dubai na bandari ya Al Hamriya.
Kufikia mwezi wanne 2008 asilimia 80 ya ardhi ya Deira ilikua tayari imekamilika
kujengwa. Muundo mpya wa muonekano wa deira ulipendekezwa na kutambulishwa
mwezi wa kumi na moja 2008.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako