Manchester united imemtolea uvivu mshambuliaji wa
timu hiyo Wayne Rooney na kumwambia kama anataka kuondoka ndani ya klabu hiyo
na kuuzwa timu nyingine basi aandike barua rasmi ya kuomba afanyiwe hivyo.
Sakata la kutaka kuondoka kwa mchezaji huyo lilianza
msimu uliopita pale mchezaji huyo alipoanza kuwekwa benchi na kocha Sir Alex
Ferguson na mara nyingine kuchezeshwa na kutolewa kitu kilichoonekana hakikumfurahisha
Wayne Rooney.
Rooney alionana na David Moyes ambaye ni kocha mpya
aliyerithi mikoba ya Sir Alex Ferguson lakini hawakuongea kwa muda mrefu juu ya
suala lao na kuonesha dalili huenda wakawa hawakuweza kufikia muafaka juu ya
mazungumzo yao.
Rooney aliwasili katika uwanja wa mazoezi wa
Manchester United unaofahamika kwa jina la Carrington lakini bado hana raha
haswa kutokana na suala lake kutofikiwa muafaka na timu hiyo.
Tayari Manchester United ilishatoa taarifa kuwa
mchezaji huyo hauzwi na b ado wangependa kumtumia na hivyo kukanusha taarifa za
kuongea na vilabu vyovyote vinavyoweza kumnunua mchezaji huyo.
Rooney anaonekana kutaka kuendelea kubaki ndani ya
klabu hiyo lakini anatakiwa mtu ambaye angekaa naye na kufanya mazungumzo ya
kumsihi atulie na Moyes ndio mtu pekee anayeonekana kuliweza hilo kwa umakini.
ROONEY AKIITUMIKIA TIMU YAKE YA MANCHESTER UNITED MSIMU ULIOPITA |
ROONEY AKIWA NDANI YA UWANJA WA CARINGTON AKIFANYA MAZOEZI |
ROONEY AKIWA NDANI YA GARI LAKE LA KIFAHARI KUELEKEA MAZOEZINI KATIKA UWANJA WA CARINGTON SIKU YA KWANZA YA KUFANYA MAZOEZI CHINI YA MOYES |
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako