Wednesday 17 July 2013

LUIZA MBUTU AWABWATUKIA DIAMOND PAMOJA NA IRENE UWOYA


KIONGOZI na mwimbaji mkongwe  wa bendi ya "Twanga Pepeta" Luiza Mbutu amefunguka na kuonyesha  kukerwa kwake na tabia ya baadhi ya wasanii wa filamu na bongofleva wanaojihusisha na skendo za kimapenzi na kuamua kuwafunda ka kuwapa somo kali.
Akizungumza na mwandishi wetu kwenye  hivi karibuni luiza alidai kwamba wasanii wa fani zote ni kioo cha jamii hivyo kitendo cha baadhi ya wasanii kujihusisha na mambo yasiyo kubalika kwenye jamii wakati wao ni kioo cha jamii  ni sawa na kuipotosha jamii hiyo inayowatazama
Mfano ishu ya Diamond na Uwoya kunaswa hotelini na mapaparazi jamii inayowatazama inawasomaje kimaisha wakati sisi wasanii ni kioo cha jamii siku hizi watu wako bize na maisha na sio mambo hayo ya kitoto kwani dunia ya sasa magonjwa ni mengi hivyo kitendo cha kubadilisha wapenzi kila kukicha ni hatari pia kwa afya yako mimi natoa somo kwa wasanii wenzangu tujiheshimu ili tuheshimike"alisema Mbutu kwa hisia kali.huku akiongeza kusema
Nashukuru kwa upande wetu wasanii wa muziki wa dansi skendo hizo za ngono sio kubwa kama ilivyo kwa wenzetu wa bongofleva na bongomovie"alisema Luiza ambaye kiukweli licha ya kuwepo kwenye fani hiyo ya muziki wa dansi kwa muda mrefu hajaingia kwenye skendo yoyote mbaya pia Luiza ni miongoni mwa wanamuziki wachache wasio na tamaa ya kuhama hama bendi kama ilivyo kwa baadhi ya wasanii wengine jambo lililopeleka kudumu kwenye cheo chake cha  ukiranja mkuu wa bendi hiyo kwa muda mrefu sasa.
Siku za karibuni msanii kiwango cha juu kwa sasa Afrika Mashariki na kati Nassib Abdul 'Diamond Platnumz' alinaswa hotel usiku wa manane na mapaparazi wa kampuni wa Global Publishers akiwa na mwigizaji nyota wa filam za kibongo lrene Uwoya ambaye ni mke wa mtu wakila raha ndani ya hotel hiyo iliyopo kando kando ya ufukwe wa bahari ya hindi jijini Dar es salaam.
 

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako