Rais wa Misri Mohammed Morsi
amesisitiza kwamba yeye ndiye kiongozi halali wa taifa huku maandamano kati ya
wapinzani na wafuasi wake yakisababisha vifo zaidi.
Rais wa Misri Mohammed Morsi |
Kwenye hotuba aliyotoa kwa taifa
usiku wa kuamkia leo, Morsi amepinga nafasi ya jeshi kutatua mgogoro wa sasa
ifikapo Jumanne. Kiongozi huyo amesema hataamrishwa na yeyote na kuwasihi
waandamanaji kuwa watulivu.
Yasadikiwa kuwa watu 16 wamekufa katika
moja wapo ya maandamano ya wafuasi wa Morsi.
Stakabathi iliyopatikana na BBC
inasema jeshi limepanga kuvunja katiba, kuweka machakato wa uchaguzi mkuu,sambamba
na kuvunja bunge la sasa.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako