Takriban
watu 41 wanadaiwa kufariki baada ya basi moja la abiria lililokuwa likitoka
Nairobi kuelekea Homabay Magharibi mwa Kenya kuanguka na kubingirikia mara
kadhaa katika eneo la Narok.
Polisi
wamethibitisha kuwa miongoni mwa waliofariki ni watoto wanne.
Mkuu
wa polisi wilayani Narok Patterson Maelo amesema kuwa dereva wa basi hilo
alishindwa kulithibiti katika eneo la kona na hivyo basi hilo kupoteza mwelekeo
na kuanguka.
Maafisa
wa shirika la msalaba mwekundi ambao tayari wamefika katika eneo la tukio hilo
wamesema kuwa watu wengine 33 waliojeruhiwa wamesafirishwa hadi hospitali ya
wilaya ya Narok kwa matibabu.
Rais
wa Kenya Uhuru Kenyatta ni miongoni wa viongozi waliotuma salamu zao za rambi
rambi kwa jamaa na marafiki wa abiria waliouawa.
Katika
ripoti iliyochapishwa katika mtandao wake wa twitter, rais Kenyatta ametoa amri
kwa idara ya polisi kuchukua hatua dhidi ya wamiliki wa magari ya umma
wanaokiuka sheria za barabarani.
SOURCE: BBC
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako