Katibu Mkuu wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dokta Willbroas Slaa
Katibu Mkuu wa Chama cha demokrasia na Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dokta Willbroad Slaa, jana alilazimika kutua kwa dharula na helikopta aliyokuwa
akisafiria, baada ya kupotea akiwa angani kwa muda wa robo saa.
Rubani aliyekuwa akiendesha helikopta hiyo, alilazimika kutua
kwa dharula baada ya kupotea eneo alilotakiwa kutua.
Tukio hilo lilitokea jana jioni wakati Dk. Slaa akitokea
wilayani Korogwe akielekea Lushoto kwenye mkutano wa kuhamasisha kuunga mkono
mapendekezo ya rasimu ya katiba mpya ambayo yanaungwa mkono na chama chake.
Dk. Slaa ambaye alikuwa atue Lushoto mjini, alipotea na kwenda
kutua mji wa Mlalo katika wilaya hiyo ya Lushoto. Kutokana na tukio hilo,
mkutano wake uliopangwa kufanyika katika wilaya ya Muheza ulichelewa kuanza.
Akihamasisha kuugwa mkono uwapo wa serikali tatu ambayo ni
Tanganyika, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano, alisema
kuwa mfumo huo hauna gharama ikilinganishwa na serikali mbili za sasa.
Aliyasema hayo jana jioni katika uwanja wa Mavi, wilayani
Muheza, alipohutubia maelfu ya wananchi wa Muheza.
Alisema kuwa serikali ya sasa ina gharama kubwa kwani ina
wabunge wengi zaidi ya 438, wakiwamo wa Zanzibar na Tanzania bara na kulipwa
mshahara mkubwa wa Sh. milioni 11 kwa mwezi.
Alisema zikiwapo serikali tatu, wabunge watapungua idadi na
kubaki 314 kwani wabunge 124 watakuwa hawapo.
Alisisitiza Rais apunguziwe madaraka na pale anapokuwa madarakani
au akimaliza muda wake, kisha ikabainika kuwa ametumia vibaya mamlaka yake
akiwa Ikulu ashitakiwe.
Katika mkutano huo, Dk. Slaa aliongozana na mratibu wa ziara,
Mwita Waitara na mjumbe wa kamati kuu Chadema Taifa, Mabere Marando.
Source: NIPASHE.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako