Milionea
Patrick Ngowi alipigiwa simu na kupewa mihadi na mwandishi wa Jarida
mashuhuri la FORBES, na mambo yalikuwa kama ifuatavyo.
Patrick
Ngowi, CEO, Helvetic Solar
Ni
majira ya saa saba na Robo mchana siku ya Jumatano ndani ya Dar es salaam,
Patrick Ngowi amekaa kwa utulivu Regency
Hotel ananisubiri tukutane kwa ajili ya mlo wa mchana, tulikubaliana kukutana
saa sita na nusu mchana lakini nilichelewa.
“Hatimaye
umefika kaka” Ngowi anatabasamu wakati anainuka kutoka kwenye kiti chake
kunikaribisha.
Ngowi
ni Mtanzania mwenye miaka 28 ambae amejenga kampuni ya solar energy yenye thamani
ya dola millioni 8. Amevaa suti nyeusi ya kupendeza na amening’iniza peni
kwenye mfuko wa suti yake, amevaa saa kwenye mkono wake wa kushoto mbayo
imeendana na viatu alivyovaa.
Ngowi
ana Historia ya kusisimua, Ni mkurugenzi mkuu wa Helvetic Solar Contractors kampuni ya kitanzania ambayo
inasambaza, kuunda na kurekebisha mifumo ya Solar kaskazini mwa Tanzania, lakini
cha kuvutia zaidi ni ukweli kwamba Ngowi amekua na mafanikio haya makubwa
katika umri mdogo. Ngowi alianza kufanya biashara akiwa na umri wa miaka 15
wakati yupo shule na alikua akifanya biashara ya vocha za mitandao yote na
wakati huo kulikua na wasambazaji wachache sana wa vocha kaskazini mwa Arusha
ambapo ndio alipokuwa akiishi Ngowi upatikanaji wake ulikuwa ni mpaka kwenye
Malls kubwa na Maduka ya simu hivyo Ngowi aligundua kuna tatizo hili la vocha
kwa majirani zake akaamua kuwasaidia. Ngowi Alichukua mtaji kwa mama yake kiasi cha shilingi elfu
hamsini akanunua vocha za jumla kwa ajili ya kuwauzia watu, Ngowi alikuwa bado
anasoma hivyo hakupata muda mwingi wa kufanya biashara yake na kuamua kuwapa
wauzaji wa sheli wamsaidie kuuza vocha kipindi ambacho yupo shuleni.
“Ilikua
sio biashara kubwa” anasema Ngowi, lakini nilipenda ukweli kwamba nilikua
natengeza hela na hivyo nikawa najitegemea kwa kiasi kidogo. Mafanikio makubwa
niliyoyapata saivi yametokana na kazi niliyokuwa naifanya kipindi cha nyuma.
Nilijifunza kuhusu faida na hasara, kutawala soko na kuajiri watu sahihi katika
biashara kwa kifupi nilijifunza vitu vingi”
Alipomaliza
elimu ya sekondari, Ngowi alikaa nyumbani mwaka mmoja kabla ya kujiunga na
elimu ya chuo. Kipindi hicho simu za mkononi zilikua ni chache na gharama sana
kwa kijana kama yeye kumiliki na ndo kipindi ambacho alifanya ziara ya kwenda
Asia ambako aligundua kuna simu za bei ya chini aliamua kuchukua mkopo kwa mama
yake kiasi cha dola 1800 na kuanza kufanya safari rasmi kati ya Tanzania na
Hongkong kununua simu za mkononi kwa watengenezaji wa gharama za chini na kuziuza
kwa wasambazaji wa simu wa Tanzania.
“Nilikuwa natengeneza kiasi kikubwa cha hela
na kipindi hicho nilikuwa na umri wa miaka 18 na miezi sita tu lakini nilikuwa
natengeneza kiasi cha dola 150, 000, maisha yalikuwa mazuri. Kutokana na safari
zake za mara kwa mara kwenda Hongkong na China Ngowi aligundua nishati ya Jua na
akajifunza kuhusu matumizi ya nguvu ya jua kwa mara ya kwanza.
Tanzania
ina tatizo kubwa la nguvu kazi kwenye miundombinu mbalimbali, kipindi cha safari
za Ngowi mara kwa mara kwenda Asia nguvu ya umeme Tanzania kwa ajili ya
kutendea kazi mbalimbali na matumizi ya nyumbani ilikuwa 10%.
Kampuni
nyingi, asasi za kiserikali na familia zenye kipato kikubwa zilitegemea sana
nguvu ya jenereta. “Tatizo la umeme Tanzania lilikua kubwa na nikafikiria kuwa
Tanzania itakuwa inahitaji nguvu ya umeme ya ziada, aliongea Ngowi huku akiinua
kinywaji chake.
Kulikuwa
na bahati na Ngowi alitaka kuitumia lakini wazazi wake walisisitiza kwamba
amalize kwanza elimu yake. Ngowi anatokea kwenye familia ya wasomi. Wazazi wake
wote ni wakufuzi.
“kuanzia
nimeanza biashara ya vocha mama yangu aliniambia nihitimu kwanza masomo yangu,
“kuacha shule sio chaguo langu, aliniweka wazi kuanzia mwanzoni” aliongea
Ngowi. Akiwa na miaka 19 Ngowi aliacha kufanya biashara na akaendelea na masomo
yake . alikuwa tayari ameshavutiwa na nguvu ya mionzi ya jua China hivyo
alienda kusoma China chuo kikuu cha Denzhou ambako alisomea nguvu ya umeme ya
kutengenezwa. Ilikuwa ni ndoa sahihi kwani alikua ameipenda china na akawa
mdadisi kuhusu nguvu ya mionzi na mafanikio ambayo inaweza kuyaleta kwa watu.
Wakati yupo
Denzhou Ngowi alianza biashara isiyo rasmi ya kusafirisha bidhaa nje ya nchi
kwani tayari alikuwa na uhusiano na baadhi ya viwanda vya ujenzi kwahiyo
alikuwa na oda kutoka kwao. “Hivyo ndio namna nilivyoweza kutengeneza mtaji wa
biashara nzima”
Mpaka
muda aliomaliza masomo yake, Ngowi alikuwa na mtaji wa kutosha, akaandaa vifaa
vya kusaidia kutengeneza umeme wa mionzi alipomaliza tu degree yake akarudi Arusha
kuanzisha biashara yake mwenyewe.
“Ghala
ya kwanza kuifungua ilikuwa ndogo lakini ilikuwa katika eneo zuri. Tulijitangaza
sana hasa kwenye shule, serikali, hospital na wengine waliopenda kutumia
nishati hii” Ngowi akaelezea
Haikuwa
rahisi wakati tunaanza, nishati ya jua haikuwa maarufu sana kwa watanzania
hivyo biashara haikwenda haraka kama tulivyodhani.
“Miezi
ya mwanzo mauzo yalikwenda taratibu” namshukuru mama kwa kuwa alinipa nguvu ya
kuendelea na biashara, kwa maneno yake ya kunitia moyo.
Kuna
wakati nilikuwa nadhani nimeingia kwenye biashara mbaya na kufikiri nitafeli
lakini mama alinishauri kuendelea, wakati mwingine ni muhimu kuwa na mtu
anayeamini unachofanya.
Ngowi
aliendelea na kuitangaza biashara yake kwa yeyote aliyefikiria atahitaji, na
baada ya vituo vya habari kupigia kampeni nishati mbadala hapo ndipo biashara
ilipoanza kushika kasi.
Kampuni
yake, Helvetic Solar ni kampuni pekee iliyopo Arusha inayotoa nishati mbadala
ya umeme wa jua. “yeyote anayehitaji nishati ya jua lazima aje kwetu, wapinzani
wengine wapo Dar es Salaam ambapo ni mbali kwa hiyo soko la Arusha lote la
kwetu.
Biashara
ilianza kuwa nzuri kwa Ngowi mwaka 2007, ambapo kampuni ilianza kuwawekea nishati
ya jua wateja wadogo wadogo na wateja wakaanza kupeana taarifa pamoja na
mawasiliano, ghafla mawakala wa serikali nao wakaanza kututafuta tuwawekee
nishati ya jua pamoja na kampuni zingine nyingi.
Mafanikio
yakaanza kuonekana mwaka 2011 ambapo mapato yalifikia Dolla za kimarekani
milioni 2.8, na mwaka 2012 dola milioni 6.8 na mwaka huu inakadiliwa mapato yatafikia
dola milioni 10.
Wateja
wakubwa wa kampuni ya Helvetic’s ni pamoja na Umoja wa Mataifa, Jeshi la
Tanzania, Shirika la WorldVision, na kanisa la Kilutherani pamoja na wengine
wengi.
Ngowi
anampango wa kupanua kampuni yake kimataifa na ameshaanza kusambaza nishati
hiyo ya jua kwa baadhi ya taasisi za kuserikali za Rwanda “Ni furuha kwetu
tumeanza kupata wateja kutoka nchi za jirani, wanapenda huduma zetu kutokana na
historia nzuri walizonazo na ubora wa bidhaa zetu,, hivyo kupata mikataba
mbalimbali,” Ngowi anaelezea
Pia
Ngowi ameweka mkataba wa takribani Dola million 5, na kampuni za utalii (Hotel
na maeneo ya kufikia wageni) mkoani Arusha
Kampuni
ya KPMG Mashariki mwa Africa imeitaja Helvetic Solar kama kampuni namba moja
inayokuwa kwa kasi katika mapitio ya kampuni 110 boranchini Tanzania kwa mwaka
2012 – 2013. Pia Ngowi yumo kati ya wagombea tuzo ya Kijana mdogo wa Kiafrika
mwenye mafanikio inayotolewa kila mwaka na Nobel.
Ngowi
amekutana na changamoto nyingi hadi kufikia hapo katika biashara yake
“natamani
kuwa na Bank moja ambayo itanihakikishia mikopo kulingana na mikataba
ninayopata, ila ni ngumu sana lingine ni miundombinu pamoja na fikra, ninafanya
kazi za umeme ambazo zinahitaji ubunifu kila mara, wakati mwingine kupata
miundombinu inakuwa ngumu hiyo inabidi niagize kutoka nje.”Anaongezea Ngowi
Changamoto
ingine aliyonayo Ngowi ni mipango yake ya kukuza mtaji wa kampuni yake kuingiza
mapato zaidi ya Dola milioni 100 ndani ya miaka mitano ijayo.
Ngowi,
Muumini wa Dini ya Kikristo ambaye anaamini sana imani yake ambayo
inamuhakikishia ya kuwa hakuna linaloshindikana chini ya jua, “ kama mungu
kanifikisha hapa, ninajua atanipeleka pale ninapofikiria kufika” anamalizia
Ngowi.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako