Tuesday, 6 August 2013

MESSI KUUZWA KWA EURO 580 MILLIONI


RAIS WA BARCELONA SANDRO ROSELL
Raisi wa Barcelona Sandro Rosell amesema klabu yake kamwe haitoweza kumuuza Lionel Messi, na alipoulizwa kama ni bei gani ambayo inaweza kubadilisha uamuzi wa klabu hiyo kwa ajili ya kumuuza alijibu kwa kifupi tu "€580 million".

 LIONEL MESS
 
RAIS WA BARCELONA SANDRO ROSELL AKIONYESHA MAPENZI YAKE KWA MCHEZAJI LIONEL MESS
Akiongea katika mahojiano na gazeti la Sport.es, Sandro Rosell alisema: “Wachezaji wote wanaweza kuondoka ikitokea tumepata ofa nzuri yenye tija kwetu lakini sio Messi. Labda tulipwe kiasi cha  €250 million ($332 million) kama ada yetu, pamoja na asilimia 56 ya fedha hizo kwa ajili ya kulipa kodi. Hivyo itabidi alipe kiasi cha  €580 million.”
Kwa maana hiyo ili kumsajili Lionel Messi itabidi klabu inayomtaka ilipe fedha ambazo ingeweza kununua vilabu viwili kama Fulham - ambayo ilinunuliwa na billionea a kimarekani Shahid Khan kwa ($230 million).
Pia kwa kauli hiyo ya Rossell inaonekana FC Barcelona wapo tayari kumuuza mchezaji yoyote kwenye kikosi chao ikiwemo Cesc Fabregas anayetakiwa na United ikiwa tu watapewa ofa itakayowaridhisha.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako