Thursday 15 August 2013

CHID BENZ ALIPOAMUA KUACHA KUTUMIA MADAWA




Rapper Chidi Benz amekiri kutumia madawa ya kulevya kwa muda mrefu, na baada ya kuzidiwa nayo ameamua kuachana nayo na kupatiwa matibabu Nairobi, Kenya.
Chidi amekiri swala hilo kupitia kipindi cha radio ya jijini Dar es Salaam pale alipofika kwa ajili ya kuachia wimbo wake mpya ambao amewaachia mashabiki kuupa jina lake.
Chidi alianza kufunguka mara baada ya kuulizwa na kuhusu ngoma hii ambayo imefanyika ndani ya wiki moja wakati alikuwa kimya mda ina maana alikuwa harikodi au?

Chidi Benzi: ngoma nimefanya nyingi sana, zingine nimetoa lakini zilikuwa hazina nguvu sana kwasababu usimamiaji ulikuwa chini na kipindi kile kulikuwa kuna mambo mengine ambayo tulikuwa tunahusika nayo yanakuchanganya akili unakuwa unafikiria mawazo mengi lakini usambazaji tu na wewe mwenyewe kujiweka kikazi nilikuwa siko hivyo.

Ulikuwa unawaza ni vitu gani ambavyo vilikuwa vinakuchanganya akili? 

Chidi Benzi: eeeh mambo mambo tu mavitu mengi unajua binaadam unakua unakutana na vitu unaonana navyo unaungana na vitu unapishana navyo, kwahiyo vitu vitu tu.

Unaweza kulizungumzia swala hilo au ni jambo umeliweka kwako binafsi?
Chidi Benzi: Aaah naweza kushare kwasababu tu familia iliniambia nisizungumzie sana  ila naweza nikashare kwasababu nilikifanya na nikaamua watu wote wapate hisia kuwa Chidi amefanya, ofcourse nilikua najihusisha na vitu vingi ambavyo ni vilevi na nini, nilikuwa nikitumia vitu vingi sana kwahiyo utumizi ule ulikuwa unanifanya saa zingine nakuwa na hasira na mawazo mengine tofauti tofauti, namchukia kila mtu na nini, kwasababu natumia vitu ambavyo vinavyozidi, naweza tukaongea na wewe  hivi story lakini nikitoka pale  namwambia wewe snich tu yaani unakuwa na hasira, kwahiyo sasa dakika ya mwisho nikagundua naficha watu au naamua kwenda kufanya kitu kwaajili ya afya yangu na maisha yangu.

 Labda jamii ingependa kujua ni vilevi vya aina gani ambavyo unavizungumzia hapa?

Chidi Benz: aaah pombe, ganja madawa na vinginevyo vinginevyo

 Kwahiyo unataka kuniambia pamoja na kwenda Nairobi pia ulikuwa umekwenda rihab pia.

Chidi: No sikua rihab ndo maana huwa sitaki kuizungumzia wala kupost kwenye ma website na nini, lakini ni kama nilienda then baada ya kufika nikakutana na Nonini kutoka airport tu gari linaanza kwenda nikagundua kwanza sikufatilia kama ulikuwa ni muda wa baridi kwahiyo nikagundua kuna baridi, then jamaa anaanza kuniambia yooo unajua tuna show kama saba, nane tisa kumi, kumi na mbili, nikamwambia show ngapi? umeniambia show kama tatu tu, akasema eeh nilikuwa nataka tu uje tunashow kama 7 nane yaani show nyingi, utaweza au unadhani kuna vitu ambavyo utavihitaji ambavyo itakuwa ngumu kwako?

 nikamwambia yaaah kuna vitu nitavihitaji, mimi bana kuna vitu navyovitumia nimefikia nikikaa twenty minutes bila hivyo vitu ni noma yaani ni noma nachanganyikiwa nakuwa akili tena sina, kwahiyo sijui tutafanyaje.akaniambia Chidi na mimi unanijua, unajua yeye nikama anakunywa pombe lakini siku mojamoja sasa unajua mi ntapataje Chidi na nairobi ni gharama,
 nikamwambia ok, nikamwambia lakini pia nnawazo lingine kuna mtu alinitonya kuwa kunakitu ambacho kinaweza kufanyika ni pesa nyingi kama milioni 15 , 16 hivi za kibongo, kama kikifanyika hicho basi nanyofolewa kabisa hivyo ambavyo vilikuwa vinanifanya niwe hivyo, akaniambia hiyo naijua lakini ni process ndio maana dunia nzima hawafanyi hiyo unaskia watu wanakufa daily na madawa hawafanyagi hiyo wewe je? 
nikamwambia mi nafanya kwasababu sasa nishakutana na vitu vingi kama ni maumivu, ni ishu aibu nishakutana nazo za mapenzi za maisha kawaida ntashindwa kufanya hicho, akaniambia watu huwa wanakufa sometimes ikikuzidia, nikamwambia ntafanya si kuna hospitali ni dawa nitafanya.
hela ikapatikana nakumbuka tuka arrange, daktari kaja kanitibia fresh, kwahiyo mi sijaenda rihab wala sijatumia methadon sijui maana zile ni mradi tu.

Sasa wewe ulitibiwa kwa njia gani?

ni dawa ambayo inanunliwa na unachomwa kama mgonjwa tu, yenyewe inakusafisha wewe pale ambapo ulikuwa ukivuta inaenda kukaa, then baada ya dakika kadhaa pakikauka panakua pakavu, ni kama ile sehem inakua ni mbichi ukivuta, lakini ukiwa huna hela huvuti panakuwa pakavu pakikauka ndio unachanganyikiwa unaanza sasa kuwa na alosto, lakini kama ukiendelea kuvuta panakuwa pabichi unaendelea, so yenyewe inaenda ni kama mapovu, panasafisha panakuwa empty ni wewe mwenyewe uamue uendelea kuvuta ama uache kabisa, lakini yenyewe inakusafisha pale kote, unaanza kuwa na power, inakupa akili, uso, rangi ya uso, mwili unaanza kubadilika, unaanza kuwa fine.,,,,,,,so niko fresh, niko healthy, nakula naishi vizuri naskia vizuri na nime-calm down.
PATAPICHA:
Hivi ndivyo ilivyo baada ya wasanii wetu kugundua madhara makubwa yatokanayo na matumizi ya madawa ya kulevya sasa wanaamka na kuzinduka usingizini. Tumeona mifano mingi kwa wale ambao wamekwisha athirika kabisa na ambao wamejinasua mapema kama dada yetu Rehema Chalamila Ray C Mungu aendelee kuwabariki na wengine ambao bado ni wanachama waache kabisa.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako