Friday 23 August 2013

AJALI YA BASI YAUA 37 NCHINI MALAYSIA


    
Takribani watu 37 wameripotiwa kupoteza maisha nchini Malaysia katika mji mkuu wa nchi hiyo Kuala Lumpur(KL) baada ya basi walilopanda kutumbukia katika korongo refu, maafisa wa usalama nchini humo wamesema ajali hii ni moja ya ajali kubwa ambazo zimewahi kutokea kutokana na kusababisha vifo vya watu wengi.
  
Baadhi ya abiria wameokolewa kutoka katika korongo hilo ambalo lina urefu wa futi 200 hali iliyosababisha waokoaji kutumia cranes pamoja na kamba kuweza kuokoa majeruhi wa ajali.
Ripoti kamili inaeleza kwamba basi hilo lilibeba abiria wapatao 49 na mpaka sasa ni abiria 16 waliokolewa wakiwa hai japokuwa hali zao bado mbaya na huenda idadi ya vifo ikaongezeka, licha ya kutokea ajali hiyo maafisa wa usalama wameshindwa kutambua uraia wa wahanga wengi wa ajali hiyo 

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako