Sunday 11 August 2013

MTOTO WA USER RAYMOND ANUSURIKA KUZAMA KWENYE POOL

Mtoto wa Usher Raymond mwenye miaka 5 amenusurika kuzama ndani ya bwawa maalum la kuogelea ambapo amewahishwa  hospitali kitengo cha watu mahututi (ICU). 
Raymond V alikuwa na shangazi yake ndani ya pool lililopo nyumbani pale alipokwama katika tundu la pool hiyo alipokuwa akijaribu kulifuata toy.
Shangazi huyo pamoja na mfanyakazi walishindwa kuutoa mkono wa mtoto huyo uliokuwa umenasa katika tundu hilo na kuanza kupiga makelele.
Wafanyakazi waliokuwa wakishughulikia Sauti na Picha katika nyumba hiyo walikimbia na kujirusha kwenye pool na kumuokoa mtoto huyo ambapo iliwalazimu kumfanyia CPR (kumkandamiza kifuani) na hatimaye kufanikiwa kumzindua.
Raymond V aliwahishwa hospitali ambapo anasemekana madaktari wamefanikiwa kurudia hali yake ya ufahamu kama kawaida na anaendelea vizuri, Usher Raymond hakuwepo nyumbani kwake wakati tukio linatokea
 
Raymond V ni mdogo wa watoto wawili wa Usher na mkewe wa zamani, Tameka Raymond, na alikabidhiwa na kupewa ruhusa ya kuwaangalia watoto wake  Agosti 2012, baada ya kutalakiana na mkewe huyo.
Mke huyo wa zamani wa Usher amepeleka hati za kisheria kuomba dharura ya kusikilizwa haraka wiki hii katika jitihada za kurudishiwa watoto wake baada ya baba yao kushindwa majukumu yake kama baba na kuwaachia watu wengine kuwaangalia watoto wake.
Ajali ya jana imetokea ikiwa ni mwaka tu tangu mtoto wa kambo wa Usher Kile Glover mwenye miaka 11 kufariki kwa ajali ya Jet Ski akiwa katika ziwa Lanier, Georgia. 

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako