Wednesday 21 August 2013

AJALI YA GARI NANE NANE MOROGORO





Mtu mmoja amenusurika kufariki baada ya gari alilokuwa akiendesha kugongana na roli katika eneo la Nane nane Oilcom barabara kuu ya Morogoro-Dar es Salaam jana usiku.
Wakizungumzia tukio hilo mashuhuda wa ajali wamemtaja Dereva wa gari dogo aina ya Prado lenye namba za usajili T 151 AXW ndio aliyesababisha ajali hiyo kwa uzembe wa kuingia barabara kubwa bila umakini wa kuangalia magari yanayopita.
"Huyu dereva wa Prado alikuwa akitokea kwenye kibarabara hiki kinachotoka shule ya sekondari ya Padri Rikodo Maria kwenye eneo hilo linalotumika kuoshea magari makubwa cha ajabu dereva huyu akaingia barabara kuu bila tahadhali na kukutana na roli hili ambalo lilikuwa kasi likishuka mteremko huu wa Oil Com kwa bahati dereva huyo wa Prado aliyekuwa peke yake alinusurika kama angekuwa na abilia mbele angekufa papo hapo kwani Lori hili liligonga upande huo wa mbele wa siti ya abiria"alisema Shuhuda huyo aliyejitambusha kwa jina la Joyce Joseph
 
Askari wa Usalama Barabarani walifika eneo la tukio na kupima ajali hiyo huku maaskari wengine wakiwa pembeni wakilinda usalama wa magari hayo.
PICHA ZAIDI ZA TUKIO HILO

SOURCE: Shekidele Blog

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako