Uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) umefungwa kwa muda baada ya moto mkubwa
kutokea katika uwanja huo mjini Nairobi, leo asubuhi.
Akielezea Mwandishi
wa BBC amesema katika uwanja huo amesema kulikuwa na moshi mkubwa uliotoka
katika eneo la kuondokea na kuingilia wageni.
Mamlaka ya uwanja
huo imesema kuwa tayari watu waliokuwa katika eneo hilo wameondolewa katika
eneo la tukio na kwa sasa moto huo umeweza kudhibitiwa.
Rais wa Kenya
Mheshimiwa Uhuru Kenyatta amewasili katika uwanja huo kuangalia hali halisi na
anatarajiwa kuhutubia waandishi wa habari baadaye ili kuelezea mazingira ya
Moto pamoja na hali ilivyo sasa.
Hadi sasa hakuna
ripoti zozote ziliotolea kuhusu majeruhi kwenye tukio hilo wala mtu aliyepoteza
maisha.
Akielezea msemaji
wa uwanja huo wa ndege James
Ole Lenku, amesema kuwa baadhi ya operesheni za uwanja
huo zimekatizwa huku ndege zinazoingia katika uwanja huo zikielekezwa kutua
katika viwanja vingine ndege kama vile Entebe, Dar es Salam, Kigali, Mombasa na
kwingineko nchini Kenya. Baadhi ya safari za ndege kutoka uwanja huo wa ndege
pia zimeahirishwa hadi hapo itakapoelezwa baadaye.
Mwishoni mwa wiki
jana baadhi ya wenye maduka ya Duty Free katika uwanja huo walifurushwa baada
ya serikali kusema kuwa leseni za wenye maduka zilikuwa zimepitwa na
muda.
Chanzo cha moto bado hakijabainika.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako