Thursday 15 August 2013

KITABU KIDOGO KULIKO CHOCHOTE DUNIANI


Hiki ndicho kitabu ambacho kwa mujibu wa rekodi, ndicho kidogo kuliko vyote duniani kutoka maktaba ya chuo kikuu cha IOWA huko Marekani vipimo vya ukubwa wake vikiwa ni inchi 0.138 katika urefu na inchi 0.04 katika upana.
Kitabu hiki ambacho kilikuwa kinadhaniwa kuwa ni Biblia wafanyakazi wa maktaba hiyo, hakiwezekani kusomwa yaliyomo ndani yake bila msaada wa kifaa cha kusaidia kukuza maandishi cheche uwezo wa hali ya juu.
 
Colleen Theisen ndiye mtu ambaye ametambulika kwa kukigundua kitabu huiki ambapo bado anaendelea na uchunguzi kuhusiana na taarifa za aliyehusika kukitengeneza, Madhumuni yake na taarifa zinazofanana na hizo.
 

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako