Monday 12 August 2013

LORI YA TANESCO YAPATA AJALI USIKU WA LEO

Gari la Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) imepinduka usiku huu baada ya kugongana uso kwa uso na gari dogo aina ya Tayota Corola katika eneo la kwa Sadala, Barabaraya Moshi/Arusha.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, gari la TANESCO ilikuwa limepakia wafanyakazi wa shirika hilo wapatao 18 wakitokea eneo la KIA kuelekea Mosh mijini.
Ameendelea kusema dereva wa gari dogo alikuwa akijaribu kuzipita gari kadhaa zilizokuwa mbele yake (zikielekea Arusha) ndipo akakutana uso kwa uso na lori hiyo ya TANESCO na alipojaribu kurudi upande wake, akawa amechelewa hivyo kugongana na gari hiyo ya TANESCO na kusababisha lori kupinduka.
Majeruhi wa ajali hiyo wamekimbizwa katika Hospital ya KCMC kuhu dereva wa gari hilo dogo akiingia mitini na kutokomea kusikojulikana

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako