Monday 5 August 2013

DEMU WA DIMOND AMZIMIA YOUNG KILLER WA "DEAR GAMBE"



KAMA  utapata fursa ya kupiga stori na masupastaa wa kike juu ya ni mastaa ganiwanaofanya music wanaowakubali basi sio ajabu kwa wao kuanza kujishebedua na kukutajia majina ya nchi za wenzetu  “Mi nampensa Drake, mi nampenda 50cents, mi nampenda Justin Bieber” hivyo ndivyo itakavyokuwa rahuisi kwao kujibu kwani siku zote ni watu  wa kujishebedua. Lakini hilo ni tofauti na demu wa Diamond Platinum maarufu kwa jina la Penny.
PENNY AKIWA DIAMOND
Alipoulizwa juu ya msanii gani anayemfagilia mdada huyo hakusita kuonesha hisia zake kwa kutaja jina la rapa chipukizi wa Mwanza anayefahamika mkwa jina la Young Killer
Penny amesema yeye na mchumba ake (Diamond wamekuwa wakipenda sana kusikiliza kazi za msanii huyo toka mwanza toka alipotoka na kazi yake ya kwanza ya Dear Gambe.

Penny aliulizwa kuhusu reaction yake katika wimbo huo ambao msanii huyo ametaja baadhi ya majina ya masupastaa wa kike huku jina la penny likiwa mojawapo.
“sasa vipi ningekuwa na penny nitakuwa free au kama ningekuwa na  mwansit wa THT ila penny nahisi Diamond atanisumbua Mwansiti pia najua pendo langu atalivua” anarap Killer.

Killer ni miongoni mwa wasanii wa Rap wanaofanya vi9izur katika soko la music wa Bongio akitamba na kibao chake cha Dear Gambe.


No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako