Thursday 29 August 2013

BAADA YA KUPIGIWA KELELE KANGA MOJA NDEMBENDEMBE BALAA JINGINE LAJA



Uchunguzi Wa kina takriban miezi kadhaa umebaini kuwepo kwa stili nyingine ya uchezaji ndembendembe, kwamba staili hiyo mpya ya uchezaji wa muziki wa mwambao kwa kulowanisha tisheti laini nyeupe kwa maji na kusababisha chuchu kuonekana sawia, inazidi kushika kasi kama moto wa kifuu Jijini Dar es Salaam.
Imebainika kuwa staili hiyo ambayo ilianzia Pwani ya Kenya, sasa inatumiwa kudhalilisha warembo Uswahilini hasa kwenye ngoma maarufu za ‘kigodoro’ ambazo huchezwa bila kujali rika mbalimbali zinazokuwa zimechanganyikana.
Habari zinaeleza kuwa katika uchezaji huo, sharti ‘nido’ ya mrembo iwe saa sita ili kuwavutia na kuwaridhisha wanaume kimahaba ambao kazi yao huwa ni kuwatuza fedha baada ya kufurahishwa kwa kutazama uchezaji huo na wengine kuondoka nao kwenda kuvunja amri ya sita.
Ilifahamika kuwa staili hiyo imewavutia wengi na vikundi vya uchezaji huo vimeanza kuundwa japo havijapata umaarufu mkubwa.
Mamlaka na wizara husika zinatakiwa kukemea kwa nguvu zote kwani huo ni mwanzo mwingine wa mmomonyoko wa maadili ya Kitanzania na ongezeko la maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU)

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako