Sunday 11 August 2013

FRANCIS CHEKA BONDIA WA TANZANIA AMTWANGA CHIOKTA CHIMWEMWE WA MALAWI KWA POINT


BINGWA wa IBF Afrika, Francis Cheka ameendeleza ubabe mbele ya mabondia wenzake baada ya usiku huu kumshinda kwa pointi Mmalawi Chiotcha Chimwemwe katika pambano lisilo la ubingwa lililochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Cheka amepata ushindi huo katika pambano hilo la raundi 8 japo baadhi ya mashabiki wamedai Mtanzania huyo amebebwa tena kama ilivyokuwa mjini Arusha alipomtwanga Chimwemwe na kutetea taji lake la IBF Desemba mwaka jana.
Ushindi huo umeendeleza rekodi ya Cheka ya kutopigwa katika ardhi ya Tanzania tangu Agosti, 2003 na kwa sasa atakuwa akijiandaa na mchezo wake mwingine lakini wa kimataifa kuwania mkanda wa WBF dhidi ya Mmarekani, Phil Williams

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako