Jopo la Madaktari Bingwa Saba wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
na Taasisi ya Mifupa ya hospitali hiyo (Moi), wamefanikiwa kuwatenganisha pacha
waliokuwa wameungana kiwiliwili.Iliwalazimu mabingwa hao kutumia saa nne
kufanikisha upasuaji huo. Mmoja wa watoto hao waliotenganishwa, amelazwa kwenye
Wodi ya Uangalizi Maalumu (ICU) Taasisi ya Mifupa Moi wakati kiwiliwili kingine
kilifariki.(P.T)
Jopo la
madaktari waliofanikisha upasuaji huo ni; bingwa mstaafu wa watoto ambaye
aliitwa maalumu kwa kazi hiyo, Petronila Ngiloi, Dk Robert Mhina (mifupa) na
Profesa Karim Manji aliyekuwa akifuatilia kwa karibu mapigo ya moyo.
Wengine ni
Dk Karima Khalid aliyekuwa akiratibu dawa ya usingizi, Dk Hamis Shaaban (ubongo
na uti wa mgongo), Dk Zaitun Bokhary (bingwa upasuaji watoto) na Dk Nyangasa
(moyo na mishipa ya fahamu)
Akizungumza
baada ya upasuaji huo, Dk Shaaban alisema walimfanyia vipimo mtoto ambaye
hakuwa amekamilika na kugundulika kuwa hakuwa amekamilika viungo vyote achilia
mbali kutokuwa na kichwa na macho pia hakuwa na moyo, figo, tumbo, maini ila
alikuwa na uti wa mgongo.
"Uti wa
mgongo ulikuwepo na ndio uliokuwa umeshikana na mwenzake na kuna mshipa mmoja
wa fahamu ulikuwa unafanya kazi ndio maana alikuwa ukimgusa anachezesha
mguu."
Alisema
kinachoratibiwa kwa sasa ni kuangalia dawa ya usingizi aliyopewa mtoto ambaye
anaendelea kupumua na kwamba ndani ya saa 24, dawa ya usingizi waliyomuwekea
mtoto huyo itakuwa imeisha na ataanza kunyonya kama kawaida.
Upasuaji
Kazi ya
upasuaji huo ilianza saa mbili asubuhi kwa mtoto huyo wa jinsi ya kike
aliyetimia kuchukuliwa vipimo mbalimbali ikiwemo CT Scan, MRI, Ultra sound na
vingine vingi kabla ya upasuaji kamili kuanza saa tano asubuhi.
Dk Shaaban
alisema ni mara ya kwanza kwa Moi kufanya upasuaji wa aina ile na kwamba mara
nyingi wamekuwa wakifanya upasuaji wa watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa
pamoja na mgongo wazi ambao tatizo hilo linasababishwa na upungufu wa madini ya
folic acid.
Kabla ya
upasuaji kuanza, mama wa mtoto huyo Pili Hija (24) alitumia muda wa nusu saa
kufanya maombi maalumu ya kumwombea mtoto wake kisha kuwaruhusu madaktari
kuendelea na upasuaji huo.
Akizungumza muda mfupi baada ya kuruhusiwa
kumwona mtoto wake, Hija alisema: "Ninamshukuru Mungu kwa yote na nazidi
kumwomba amjalie mwanangu apone kabisa, nawashukuru na nitazidi kuwaombea
madaktari wanaomtibu mwanangu."Alijifungulia nyumbani Agosti 18 maeneo ya
Jang'ombe, Zanzibar watoto pacha walioungana mmoja akiwa amekamilika viungo
vyote na mwingine akiwa na kiwiliwili.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako