Thursday 29 August 2013

AUNT EZEKIEL APIGWA CHUPA NA KUPASUKA MKONONI

                             
MWIGIZAJI wa  sinema za kibongo, Aunt Ezekiel Grayson ‘Gwantwa’ amenusurika kupasuliwa paji la uso kwa chupa baada ya kupigwa mkononi, Jumapili usiku.
Aunt Ezekiel alimpiga na chupa tupu ya bia na kumpasua katika mkono wa kushoto na mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Yvonne Bigirwa, nje ya Ukumbi wa Billicanas wakati wa show ya muziki iliyoandaliwa na Endless Fame ambapo walikuwa wakiwatambulisha wasanii wao pamoja na Nyimbo zao mpya.
Watu walioshuhudia tukio hilo wamedai kuwa, wakati Yvonne anatekeleza ukatili huo, Aunt alikuwa amesimama na marafiki zake waliotajwa kwa jina moja moja, Sajenti na Rehema.
“Ndani ya ukumbi shoo ilikuwa ikiendelea, Aunt, Rehema na Sajenti walisimama nje, ghafla alitokea Yvonne akiwa na chupa mkononi, akailenga kwenye paji la uso la mwenzake, bahati nzuri Aunt aliiona na kukinga mkono,” kilisema chanzo.
Aliongeza, Vurugu kubwa ilizuka, ilibidi shoo ndani isimame ili kushughulia suala hilo ambapo baada ya vurugu kutulia Aunt alikimbizwa Aga Khan huku Yvonne akapelekwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Dar ambapo anashikiliwa hadi sasa.
                          
Baada ya taarifa hizo, Jumatatu mchana mwandishi wetu  alifika  nyumbani kwa Aunt, Mwananyamala na kumkuta ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Ishu ni kweli kama mlivyosikia, lakini kule Agha Khan sikutibiwa, niliambiwa daktari hayupo mpaka saa mbili asubuhi na muda huo ilikuwa saa kumi alfajiri.
                           
“Ilibidi niende kutibiwa kwa Dokta Mvungi, Kinondoni Hospitali ambako nilishonwa nyuzi sita.”
mwandishi: Madai ya Yvonne ni nini hasa?
Aunt: Yaani hata mimi sijui, nilishangaa sana. Kwanza lengo lake lilikuwa kunijeruhi kwenye uso, lakini niliiona chupa nikaikinga na mkono ndiyo maana ikaniumiza.
Huyu ndiye Yvonne aliyempiga chupa Aunt Ezekiel
mwandishi: Siku za nyuma uliwahi kuingia kwenye mzozo na Yvonne kwamba unamchukulia mpenzi wake aitwaye Joff, siyo kwamba ndiyo kisasi?
Aunt: Yale mambo yalipita, yeye ana maisha yake na mimi nina yangu.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako