WAKATI
Waislamu wakiwa ndani ya Mfungo wa Mwezi Ramadhani, mapenzi yamepelekea
kifo cha kijana Ibrahim Ibrahim ‘Ibra’ wa Kundi la Wakali Danta la Magomeni
jijini Dar kwa kuchomwa na kisu mara mbili.
MAREHEMU IBRAHIM ENZI ZA UHAI WAKE
“Siku ya
tukio Kelvin alikutana na Fatma, akamuanzishia vurugu akimuuliza sababu ya
kumuacha yeye ili aolewa na Ibra. Vurugu ilikuwa kubwa, Fatma akaamua kumuita
Ibra ili amsaidie.
“Ibra alipofika ndipo akaanza kupigana na Kelvin, kuona amezidiwa Kelvin alitoa kisu na kumchoma cha kwanza kisha cha pili hapo Ibra akaanguka chini na hakuamka tena,” alidai mtoa habari huyo ambae hakutaka jina lake litajwe.

Baada ya
tukio hilo inadaiwa Kelvin na Fatma walikimbia,
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Camilius Wambura alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo lilitokea Julai 27, saa 9:30 eneo la Brazil Magomeni Kagera.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Camilius Wambura alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo lilitokea Julai 27, saa 9:30 eneo la Brazil Magomeni Kagera.
Kamanda Wambura alisema kuwa Kelvin ambaye anahusika na mauaji hayo anasakwa na jeshi la polisi.
Mbali na Kelvin pia mwanamke ambaye ndiye chanzo cha tukio hilo naye anasakwa.
Kesi hiyo imefunguliwa jalada namba MAG/IR/5600/ 2013 MAUAJI.
Uchunguzi wa jeshi la polisi unaendelea zaidi ili kuweza kuwakamata wahusika waweze kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
MWILI WA MAREHEMU UKIPELEKWA MAKABURINI
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako