AC Milan ya
Italia kwa mara ya kumi na moja katika muda wa miaka kumi na mbili iliyopita
imefuzu kushiriki Kombe la Klabu Bingwa baranai Ulaya.
Milan
imeilaza PSV Eindhoven kutoka Uholanzi kwa mabao 3-0.
Baada
ya kutoka sare ya 1-1 na Uholanzi katika mechi ya awamu ya kwanza, Kevin Prince
alifunga mabao mawili yaliyoiweka timu yake mbele, naye Mario Balotelli
akaongezea la tatu na hivyo kuihakikishia mabingwa wa zamani wa kombe hilo
nafasi katika raundi ijayo kwa jumla ya mgoli 4-1.
Katika
matokeo mengine iliyochezwa siku ya jumatano, Zenit St Petersburg iliikwaruza
Pacos Ferreira kwa mabao manne kwa mawili na kufuzu kwa hatua ijayo kwa jumla
magoli manane kwa matatu.
Kwingineko,
mabingwa wa Jamhuri ya Czech, Viktoria Plzen walishinda wenyeji wao Slovenia
Maribor kwa bao moja kwa bila na kujikatia tikiti ya raundi ijayo ya makundi ya
kinyang'anyiro cha kuwania Kombe la Klabu Bingwa Barani Ulaya.
Viktoria
Plzen imesonga mbele na jumla la magoli 4-1.
Klabu
hizo zitajiunga na Arsenal Schalke, Steaua Bucharest na Austria Vienna ambazo
zote zilishinda mechi zao siku ya Jumanne katika hatua ya makundi.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako