Saturday 17 August 2013

BILIONEA ROSALIA AFARIKI DUNIA

Watu wengi mtakuwa mnaifahamu brand ya Zara maarufu sana kwenye dunia ya fashion, lakini watu ambao wako nyuma ya brand hii wanaweza wasiwe maarufu. Rosalia Mera ambaye hadi anafariki alikuwa na utajiri wa dola billioni 6.1 ambazo zinatokana na kuwa mmoja ya waanzilishi wa brand ya Zara akiwa na mme wake Amancio Ortega mwenye utajiri wa dola billioni 57.
Vyanzo vya habari vinasema kwamba mama huyu alikuwa likizo na mwanae ambapo alipatwa na ugonjwa wa uliotajwa kama “Brain hemorrhage”, baadaye alifariki dunia. Rosalia Mera akiwa na umri wa miaka 11 aliacha shule na baadae walianza kutengeneza magauni wakiwa nyumbani kwao na mme wake Amancio Ortega na hapo ndiyo mwanzo wa Zara. Rosalia Mera raia wa Hispania amefariki akiwa na miaka 69.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako