Katika hali isiyo ya kawaida, Wanaume wawili nchini Kenya
wameibuka na mbinu isiyo ya kawaida ya kupata suluhu ya kupigania mwanamke
ambaye wote wanampenda Wamesaini mkataba wakikubaliana kuishi nae kwa
zamu.
Silvester Mwendwa ni mmoja wa wanaume hao anayeanza kwa kueleza
kwa nini binafsi anamuhusudu mwanamke huyo.
Mmoja wa wanaume hao alisema haoni ubaya wowote kwa yeye na
mwenzake kumuoa mwanamke mmoja.
Amehoji sheria ya sasa inayoruhusu wanaume kuoa wanawake wengi
na wakati huo huo kuharamisha mpango kama huo kwa kina mama.
Sylvester Mwendwa anasema wazazi wake wamekubali na mpango wake
na wako tayari kumtolea mahari.
Wanaume hao wawili walikubali kumuoa mwanamke huyo baada ya
kugundua kwamba kumbe wote wana uhusiano wa kimapenzi naye.
Na kumbe mwanamke huyo alikuwa ameahidiana na kila mmoja wao
kwamba angelifunga nao ndoa bila ya wao kujuana.
Lakini walipogunduana, ilikuwa ni ugomvi wa mara kwa mara lakini
mwanamke huyo alipoambiwa amchague mmoja wao alishindwa akisema anawapenda wote
wawili
Na baada ya hapo watatu hao waliafikiana kusaini mkataba ambao
utaruhusu wanaume hao wawili kuishi na mwanamke huyo kama bwana na bibi ila
kila mmoja wao atakuwa na wakati wake wa kwenda kumjulia hali.
Vile vile mkataba huo unawashurutisha kugawana majukumu yote ya
nyumbani ikiwa ni pamoja na kuwalea watoto na kutowabagua kwa kuwa wote
watakuwa na haki sawa.
Hata hivyo kwa mujibu wa sheria za
kenya ni haramu kwa mwanamke kuolewa na wanaume wawili na mkataba huo sasa
umeibua mjadala mkali wa kisheria, huku sheria mpya ya ndoa ikitarajiwa
kujadiliwa na kuidhinishwa bungeni.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako