Friday 23 August 2013

2 CHAINZ AKAMATWA NA POLISI NA KUWEKWA KIZUIZINI

 Msanii 2 Chains ni mmoja kati ya watu 11 waliokamatwa na Police baada ya kukataa kutoka kwenye basi walilokuwa wakisafiria kutoka Mji wa Oklahoma mapema Alhamisi ya wiki hii. 

2 chainz ambaye jina lake halisi ni Tauheed Epps, na wenzake wamekamatwa na polisi baada ya kukaidi amri ya taa za kuongozea magari alhamisi asubuhi” amesema Sajenti Jennifer Wardlow
Ila hadi kufikia Mchana wa siku hiyo wote 11 walifanikiwa kulipa faini ya $ 2,000 za kimarekani ambazo ni sawa na shilingi milioni 3 na laki 6 na waliachiwa kutoka kizuizini aliongeza msemaji wa polisi kituo cha Oklahoma Mark Mysers.
2 Chainz mwenye umri wa miaka 35 alikuwa kwenye onyesho pamoja na Lil Wayne na T.I huko mjini Oklahoma usiku wa Jumatano, wakati wanarudi ndio polisi walilisimamisha basi alilokuwemo 2 Chainz.
Dereva wa basi hilo pia alikamatwa wakati akijaribu kutoka ndani ya basi hilo. 
Watu hao 11 walikaidi kutii amri ya polisi hao wa Oklahoma kwa takribani masaa kadhaa kitendo kilichosababisha wapelekwe ndani “kizuizini”
Hadi sasa wachunguzi hawajampata mmiliki wa basi hilo, na kutokana na maelezo kutoka kwa msemaji huyo wa polisi mashtaka mwengine yatafunguliwa baadaye, baada ya kukamilika kwa upelelezi.
Msanii 2 Chainz aliyekulia Mjini Atlanta, mwanzo alijulikana kwa jina la Tiny Boi alipokuwa mmoja kati ya wanakundi la Playaz Circle kabla ya kufanya kazi pekeyake, ambapo mwaka 2012 alitoa albam yake iliyokwenda kwa jina la “Based on a T.R.U Story” iliyoingia kwenye chati za Billboard. Pia albam yake mpya inayokwenda kwa jina la “B.O.A.T.S.II: Me Time” ambayo amepanga kuitoa mwezi ujao.
 
Mwanzoni mwaka huu 2 Chainz alituhumiwa kukutwa na Bangi na kufunguliwa mashtaka baada ya kukamatwa akitoka Maryland’s Eastern Shore

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako