Msanii wa Bongo fleva Mabeste mwaka
huu anashukuru mungu baada ya wife wake kujifungua salama mtoto wa kiume.
"Mabeste" Nashukuru ndugu zangu
na marafiki zangu kwa ushirikiano mnaonionesha toka mwanzo mpaka sasa, muda
mrefu nilikua kimya kwa ajili ya majukumu ya kifamilia.
Mabeste kwa mara ya kwanza anatarajia
kufanya show yake ya kwanza baada ya kupata mtoto wa kiume siku ya Idd mosi
jijini hapa ili kuonyesha mapenzi aliyonayo juu ya mtoto wake, na kuwashukuru
ndugu zake na marafiki kwa kuwa haikuwa rahisi kupata mtoto huyo na ukizingatia
ni mtoto wake wa kwanza.
Siku kuu ya Idd mosi msanii huyu atakuwa
katika viwanja vya Dar west park Tabata kwa ajili ya kuonyesha ukali alionao
pamoja na kuachia ngoma zake kama Baadaye sana, Dole na nyingine kibao kwa
kiingilio cha elfu 5 tu kuanzia saa 3 usiku mpaka majogoo kama hiyo haitoshi
kutakuwa na wasanii wengine kibao wa bongo fleva.
Pia Mabeste amewataka mashabiki wake wakae
tayari kwa ujio wake mpya baada ya kusherehekea sikukuu ya Idd mosi Dar west
park Tabata.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako