Siri ya Yanga kugomea mkataba wa
udhamini wa Azam TV, inadaiwa ni kutokana na klabu hiyo ya mtaa wa Jangwani
kuwa na mazungumzo na Kampuni ya Zuku TV kwa ajili ya kuonyesha kipindi cha
Yanga.
Habari za uhakika ambazo tumezipata kutoka
kwa kiongozi mmoja wa Kamati ya Utendaji ya Yanga zinasema kuwa Zuku wapo
tayari kutoa Sh 400 milioni kudhamini kipindi cha Yanga ‘Yanga TV Show’.
“Mazungumzo ya awali yalikuwa na ofa
ya Sh 300 milioni, sasa wamekuja na ofa ya Sh 400 milioni ndiyo ipo mezani,
mazungumzo yanaendelea,”kilisema chanzo hicho.
Iwapo watakubaliana, mashabiki wa
Yanga watapata fursa ya kuona programu za mazoezi ya timu yao, mahojiano ya
wachezaji, makocha, viongozi na masuala mbalimbali ya maendeleo ya klabu ya
Yanga.
Chanzo hicho kimedai kuwa mazungumzo
hayo ya chini kwa chini yanayoendelea baina ya Yanga na Zuku ndiyo
yanasababisha klabu hiyo ya Jangwani kukataa ofa ya Azam ambayo hivi karibuni
iliingia mkataba na Simba wenye thamani ya Sh 331 milioni kwa muda wa miaka
mitatu huku Yanga wakikalia kimya ofa yao.
Hata hivyo msemaji wa Zuku, Julie
Kalanje alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema kwa kifupi, “Kuna mambo mengi,
lakini kwa sasa mwenye haki za TV ni Azam, hakuna mazungumzo yoyote
yanayoendelea na Yanga ila muda muafaka ukifika kuzungumzia jambo hilo
tutawaambia.”
Naye Katibu wa Yanga, Lawrance
Mwalusako alisema hakuwapo kwenye mkutano wa majadiliano na Zuku.
Madai mengine ya Yanga kukataa
mkataba wa udhamini wa Azam TV, ni kipengele cha CD za mchezo ambazo Azam
watazimiliki, ambapo Yanga watakapozihitaji hawatapewa, pia suala la udini
ambalo wanadai Azam walishawahi kugomea kushiriki michuano ya Tusker kwa kile
walichoeleza yamedhaminiwa na kampuni ya pombe, ambapo hivi sasa Yanga
inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Hata hivyo Mwenyekiti wa Kamati ya
Ligi, Wallace Karia akizungumzia suala hilo alisema madai hayo ya Yanga hayana
mashiko kwani klabu zote zitapewa CD za kila mchezo na pia suala la TBL
kuidhamini Yanga siyo peke yao ambao wanadhaminiwa na TBL kwani hata Simba nao
wadhaminiwa na TBL na tayari wameishakubaliana na Azam TV.
“Kwanza mpaka sasa hatujasaini
mkataba wowote, kilichopo mezani ni mkataba wa maelewano vikao vyote kwa upande
wa Yanga wameshiriki Mwalusako (katibu) na Sanga (Makamu) sasa tunashangaa
wanasema hawajashirikishwa,”alisema Karia.
hiyo kwa kumtaka Rais wa Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga kuingilia kati na kukaa mezani na
viongozi wa Yanga ili wamalizane kwa njia ya amani.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako