JUHUDI za Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe za kupambana na
dawa za kulevya nchini Tanzana zimeanza kuzaa matunda baada ya jana
akiwa katika ukaguzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Julius Nyerere
kunaswa kijana akijaribu kupita na dawa za kulevya katika uwanja huo.
Kwa
kile kuoneshwa kukerwa na tabia hizo, Dk. Mwakyembe amempiga picha
kijana huyo ambaye ni rasta na picha yake itasambazwa maeneo tofauti,
huku kesi yake ikiendelea ya kupatikana na madawa hayo ya kulevya.
Akizungumza
na vyombo vya habari leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Dk.
Mwakyembe alimtaja kijana aliyekamatwa jana kuwa ni Leonard Jeremiah
Monyo (Edwin Jeremiah Monyo) ambaye amekamatwa na kete 86 za madawa ya
kulevya aina ya heroin akitaka kusafiri nazo kuelekea Italy misokoto ya bangi
34 akiwa ameficha kwenye begi lake.
Alisema
kijana huyo rasta alinaswa na mtambo wa kukagua mzigo baada ya wakaguzi
kuushuku mzigo wake hivyo kuamuru ukaguliwe ndipo alipokutwa na madawa
hayo haramu akijaribu kusafiri nayo kwa ndege.
Alisema
kijana huyo kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi
zaidi kabla ya kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kukutwa na dawa
hizo haramu. Alisema kwa kile kuoneshwa kukerwa na vitendo hivyo na
kuamua kwa dhati kupambana navyo wamempiga picha kijana huyo na picha
zake zitasambazwa maeneo mbalimbali ili aonekane na umma kujua watua
ambao wamekuwa wakilichafua taifa nje na ndani kutokana na biashara hizo
haramu.
Dk. Mwakyembe
amesema atahakikisha anafuatilia kesi ya kijana huyo hadi itakapoishia
ili kuona hatua za kisheria zinachukuliwa kwa wahusika na vitendo hivyo
kukomeshwa. Alisema maofisa wakaguzi wa mizigo wawili (wote wasichana)
ambao walimnasa kijana huyo watazawadiwa na kupandishwa daraja kutokana
na kazi nzuri waliyoifanya.
"Jana
tu baada ya ukaguzi wenzetu ambao wanaona kama tunafanya mzaha jana
tena wakapitisha mzigo wa madawa ya kulevya kiwanja cha ndege cha Dar es
Salaam, kwa sababu vijana wetu sasa wameamka na hawataki mchezo
wakamkamata kijana huyo...," alisema.
"Picha
yake itasambazwa kila sehemu...sidhani kama tunahitaji upelelezi kwa
sababu tumekukamata na dawa za kulevya. Mimi na viongozi wangu kupitisha
dawa za kulevya akikisha kuuhakikisha.
Alisema
kijana huyo alikamatwa majira ya saa mbili na nusu usiku akiwa
anasafiri kwenda nchini Italia kwa kutumia ndege ya kampuni ya Swissair.
Alisema kwa sasa kila atakayekamatwa na dawa za kulevya picha yake
itasambazwa maeneo mbalimbali ya nchi ili watu hao wajulikane.
Alisema
kwa sasa taratibu zinafanywa ili kuhakikisha mizigo ya abiria
wanaowasili kutoka nje ya nchi kuingia Tanzania nao mizigo ikaguliwe ili
kuwabaini wanaoingiza bidhaa hiyo haramu ichini pia. Aliongeza zoezi
hilo litafanyika katika viwanja vya ndege na bandarini kwa kila mizigo
inapowasili.
Alisema
lengo ni kuhakikisha viwanja vya ndege vinakuwa salama na kuacha
kutumika vibaya na baadhi ya watu, jambo ambalo limeendelea kulichafua
taifa. Alisem kiwanja cha Dar es Salaam ni kizuri na kina vifaa vya
usalama vya kutosha ila mapungufu yaliyopo ni kwa baadhi ya wafanyakazi
ambao wanatumia vibaya madaraka yao.
Dk.
Mwakyembe ameahidi kuwataja na kuweka picha zao hadharani watu ambao
wanajihusisha na madawa hayo ya kulevya. Amesema wanatarajia kutaja
majina ya Watanzania ambao hivi karibuni walinaswa na dawa za kulevya
nchini Afrika Kusini katika uwanja wa ndege wa Oliver Tambo. Alisema
Watanzania wengine wamekamatwa Hong Kong wakihusishwa na dawa hizo na
wanafuatilia pia picha na majina yao yatawekwa hadharani muda wowote.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako