Tuesday 27 August 2013

PHD AKIWA HOSPITAL BAADA YA KUPATA AJALI

Superstar wa mjini, Muigizaji Hemedy Suleiman a.k.a PHD ambaye pia ni mwanamuziki wa Bongofleva amefunguka kuwa anaendelea vizuri baada ya kupata ajali mbaya ya gari na gari hilo kuharibika.
Hemedy alikuwa akimsindikiza Gerry Wa Rhymes ambaye pia ni msanii maarufu nyumbani kwake Sinza na wakati akirusi nyumbani kwake alipata ajali baada ya kugonga kalivati lililopo pembeni ya mtaro maeneo ya Kijitonyama Kisiwani.
 
Hemedy ameumia kwenye paja na kifuani ambapo Staring ilimbana na kwa sasa yupo Hospital akiendelea na matibabu na Kupitia mtandao mmoja wa kijamii Hemedy ameandika "Namshukuru mungu naendelea vizuri baada ya kupata ajali mbaya iliyonikuta, ahsanteni kwa dua zenu, kifua tu ndiyo kimeumia na mkono"

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako