Saturday, 3 August 2013

MWANDISHI WA CHANNEL 10 APIGWA NA ASKARI

Eliah Ruzika akiwa amefungwa pingu mkononi baada ya kukataa kutoa Mkanda wa Video aliourekodi wakati wa Vurugu maeneo ya Tazara Jana Jioni

MWANDISHI NA MPIGA PICHA WA CHANNEL TEN ELIAH RUZIKA AMEPIGWA NA ASKARI WA JESHI LA POLISI AKIWA KAZINI KWENYE MKUTANO WA WAFANYAKAZI WA TAZARA, ALIPOONA VURUGU ZIWAWEZA KUTOKEA MKUTANONI, ALIAMUA KUONDOKA KUMBE ASKARI WALIKUWA WAKIMFUATILIA NYUMA YAKE NA ALIPOFIKA MAENEO YA TRAFFIC LIGHT ZA TAZARA ASKARI HAO WALIMVAMIA NA KUMKAMATA NA KUANZA KUMPIGA NA KUMLAZIMISHSHA AWAPE MKANDA ULIOREKODIWA KWENYE TUKIO, NDIPO ALIPOGOMA NA WAKAANZA KUMPA KICHAPO AKIWA WAMEMFUNGA PINGU. NI RAIA WEMA NDIO WALIOMUOKOA NA KUMFUNGUA PINGU HIZO…AHSANTENI RAIA WEMA KWA HILI. TUNASIKITIKA SANA KUONA KWAMBA WOTE TUNAITUMIKIA SERIKALI MOJA LAKINI WENGINE WANATUMIA VIBAYA MAMLAKA WALIYONAYO. KWA BAHATI NZURI UKANDA WALIOUTAKA HAWAKUUPATA NA PICHA ZA ASKARI WALIOFANYA TUKIO HILO ZIPO ILA HATUKUZIWEKA HADHARANI KWA MAKUSUDIO MEMA.
Taarifa Na Dj Cue kutoka Magic Fm

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako