Thursday 8 August 2013

RAIA ALIYEPIGWA RISASI NA MAJAMBAZI AFARIKI DUNIA

MAREHEMU PATRICK RWEYOMBAZI
Mhadhiri wa College of Engeneering katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, UDSM, Patrick Rweyongeza, amefariki mara baada ya jana kupigwa risasi na majambazi maeneo ya Magomeni.

Tukio hilo limetoke maeneo ya magomeni usalama nje ya jengo la Benk ya Biashara zamani ikijulikana kama Benk ya Wananchi majira ya mchana wa tarehe 7/8/13 

Kama PATA PICHA ilivyohabarisha kuhusiana na tukio hili tangu kutokea kwake mpaka sasa majambazi hao hawajaweza kupatikana. Vyombo vya dola vimeombwa kuwa makini na kuyafanyia uchunguzi wa kina matukio kama haya ambayo kwa kipindi cha karibuni yameeonekana kufululiza hapa nchini, mfano kifo cha tajiri wa mererani aliyepigwa risasi na kufariki papohapo.
MWILI WA MAREHEMU UKIWA JUU YA LORI KUPELEKWA HOSPITALI

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako