JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro limemkamata
mfanyabiashara mashuhuri wa mjini Moshi, Totolii Kimath anayedaiwa kurekodi
mkanda wa video ukimwonyesha akimlawiti mfanyakazi wake wa dukani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz,
aliliambia Tanzania Daima kuwa kijana huyo ambaye anamiliki maduka ya kuuza na
kutengeneza CD katika kituo kikuu cha mabasi cha mjini Moshi, alikamatwa katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), akitokea Dubai.
Alisema Jeshi la Polisi lilikuwa likifanya uchunguzi
kwa muda mrefu wa picha zilizosambaa katika mitandao ya kijamii na simu ambazo
zinaonyesha mwanaume na mwanamke wakifanya mapenzi kinyume cha maumbile
“Tulikuwa tunafanya uchunguzi wa picha zilizosambaa
kwenye mitandao pamoja na simu kwenye Whatsapp ambazo zinaonyesha watu
wakifanya mapenzi kinyume cha maumbile, kimsingi ni kosa la jinai mwanamke
kumruhusu mwanaume amuingilie kinyume cha maumbile ama mwanaume amuingilie
kinyume na maumbile,” alisema.
Alisema bado uchunguzi wa picha hizo unaendelea ikiwa
ni pamoja na kumhoji mhusika na kwamba endapo uchunguzi utakamilika atafikishwa
mahakamani kwa kosa la kushiriki kufanya mapenzi kinyume cha maumbile.
Kifungu namba 154 cha kanuni ya adhabu kimeweka
adhabu ya kifungo cha maisha kwa mtu anayepatikana na hatia ya kufanya mapenzi
na mtu mwingine kinyume cha maumbile.
Video za mfanyabiashara huyo ambazo zimekuwa gumzo
zimekuwa zikisambazwa kupitia mitandao ya simu hususan Whatsapp na nyingine
zikiuzwa katika maduka yaliyopo stendi kuu ya mabasi Moshi.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili ulibaini kuuzwa
kwa video hizo ambazo zina vipande viwili, kimoja kikiwa na urefu wa dakika
8:47 na kingine dakika 4:00 kwa kiasi cha kati ya sh 3,000 hadi 5,000 katika
maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi.
Inadaiwa kuwa mfanyabiashara huyo kijana anayemiliki
maduka matatu Stendi Kuu ya Mabasi, alirekodi video hizo kwa siri bila
mfanyakazi wake huyo kujua na kuihifadhi kwenye kompyuta ambazo moja kati ya
vipande hivyo inaonyesha akimlawiti mfanyakazi wake huyo.
Katika hatua nyingine, taarifa mbalimbali kutoka eneo
la stendi kuu ya mabasi zinasema baadhi ya wasichana wanaodaiwa kufanya mapenzi
na kijana huyo wameingiwa na hofu kutokana na video nyingine ambazo zinadaiwa
kurekodiwa na kijana huyo akifanya mapenzi nao.
“Hapa stendi sasa hivi mabinti waliotembea na jamaa
wako roho juu maana tayari nimesikia mshikaji alikuwa akirekodi kila msichana
aliyetembea naye, sasa wana hofu kuwa video zao pia zitasambaa kama zilivyokuwa
hizi nyingine,” alisema kijana mmoja muuzaji wa duka la CD ambaye hakupenda
jina lake kutajwa gazetini.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako