Mtu aliyetambuliwa kuwa
Mtanzania yumo hatarini ya kufungwa miaka 40 jela nchini Marekani baada ya
kukamatwa na dawa za kulevya dawa aina ya heroin zikiwa ndani ya kompyuta
pakato (laptop).
Shirika la habari la The Associated
Press tarehe 15 Agosti 2013 limechapisha habari hiyo na kusema kuwa Mtanzania
huyo ametambulika kwa jina la Joseph Mackubi (miaka 33), alikamatwa katika
kiwanja cha ndege cha LAX mjini Los Angeles akitokea Nairobi.
Mackubi alipandishwa atika kizimba cha
mahakama (Federal court) jijini LA na kusomewa mashitaka siku ya
Jumatano, Agosti 14, 2013 ambapo
alikiri kukutwa na dawa hizo zilizokuwa zimefichwa kwenye laptop isiyofanya
kazi.
Inaripotiwa kuwa maafisa waligundua
uzito usio wa kawaida wa laptop aliyokuwa nayo Mackubi mwezi Oktoba mwaka jana
walipompekua. Walipompeleka kumpekua kwa mara ya pili kwa kina zaidi,
walijaribu kuwasha komyputa hiyo bila mafanikio, na kugundua kuwa ilikuwa ina
alama za kufunguliwa awali (tampered with), na ndipo walipoifungua kabisa ndani
ambapo walikuta gramu 800 za heroin zimefichwa.
Mackubi alisema alikuwa akutane na
mwanamke anayeishi jimboni Alabama, ambaye walifahamiana kwenye mtandao wa
internet. Maafisa wamesema kuwa Watanzania ni miongoni mwa watu wanaokamatwa
LAX wakisafirisha dawa za kulevya kwa njia hiyo.
Hukumu impasayo Mackubi imepangwa
kutolewa tarehe 11 Septemba mwaka huu
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako