Thursday 8 August 2013

RAIA APIGWA RISASI NA MAJAMBAZI MAGOMENI DAR ES SALAAM

KIJANA ALIYEPIGWA RISASI AKIWA JUU YA GARI TAYARI KUPELEKWA HOSPITALI
MtU Mmoja aliyekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25-35 amepigwa risasi ubavuni na majambazi maeneo ya magomeni usalama nje ya jengo la Benk ya Biashara zamani ikijulikana kama Benk ya Wananchi majira ya mchana wa tarehe 7/8/13
Chanzo chetu cha habari kutoka kwa mwandishi aliyekuwa kwenye eneo la tukio kinaelezea kuwa; majambazi hao walikuwa kwenye pikipiki 2 aina ya Boks ndipo wakawa wanamfata raia huyo ambae jina lake halikuweza kupatikana aliyekuwa ndani ya gari lake aina ya Opah wakimfatilia kwa nyuma nyuma huku pikipiki moja upande  wa kulia na nyingine kwa nyuma upande wa kushoto.
Akiwa kwenye foleni wakamuamuru awape pesa ndipo raia huyo akawapatia bahasha. Mara baada ya kupokea bahasha hiyo ya kaki jambazi mmoja aliyekuwa kwenye pikipiki upande (kulis) aliokuwa dereva akampiga risasi ya ubavu iliyopelekea damu nyingi kumwagika na kupoteza fahamu.

JINSI DAMU ILIVYOKUWA INACHURUZIKA
Majeruhi alipatiwa huduma ya kwanza mara baada ya majambazi kukimbia na kuwahishwa hospitalini kwa ajili ya kuitoa risasi iliyozama ndani ya mwili wake ili kunusuru maisha ya kijana huyo mwenye asili ya watu kutoka kaskazini Arusha.
Baadhi ya picha eneo la tukio na raia aliyejeruhiwa kwa risasi unazipata kupitia mtandao wa habari.(Habarika Vyema )
LORI ILIYOMBEBA KIJANA ALIYEPIGWA RISASI NA MAJAMBAZI

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako