Friday 23 August 2013

JOKATE AZUNGUMZA MAMBO YANAYOFANYA WANAUME WAMPENDE

Mrembo anayefanya vizuri katika mambo mengi sana nchini Jokate Mwegelo amezungumza na kutaja Mambo manne yanayomfanya apendwe sana na wanaume wengi hapa nchini.
1. Kujiamini
Hii ndio sababu kubwa ya kwanza aliyoitaja Jokate. Anasema hamna kitu kinachowavutia watu, hasa wanaume kama kujiamini. Mwanaume anapenda msichana anayejiamini. Zaidi ya yote hamna kitu kinachosema kuwa “I’m sexy” Zaidi ya mwanamke anayejiamini
2. Kujitegemea
Hii ni kama sababu ya kwanza hapo juu,  Jokate anasema hamna kitu kinachowaboa wanaume kama mwanamke ambaye anapenda vitu vya kupewa. Ukimuonesha mwanaume wewe unapenda kutafuta vya kwako basi jua atakupenda sana
3. Kupendeza
Jokate anasema ni muhimu kwa wadada kuvaa nguo nzuri ambazo zitakupendeza kulingana na mwili wako hasa hasa nguo zenye rangi ya kuonekana.
4. Tabasamu
Tabasamu kila saa kwani tabasamu linakufanya unaonekana mzuri Zaidi


No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako