Monday 12 August 2013

DUDE ASEMA WASANII HAWANA KITU

MTAYARISHAJI na Muongozaji wa filamu nchini Tanzania Swahilihood Kulwa Kikumba DUDE anasikitishwa na wasanii wa filamu kutojielewa hadi leo na kuendelea kuishi maisha ya kubahatisha wakati wao wenyewe wanaweza kuamua maisha yapi wanaweza kuishi kuzingatia na hali halisi ya maisha yalivyo sasa.
Haya naongea na hata mimi yananihusu sisi wasanii wafilamu hasa watayarishaji hatujitambui wala hatujielewi, na ndio maana maisha yetu yamekuwa magumu na kuishia katika nyumba za kupanga kama si nyumba za familia zetu na magari ya kukodisha pamoja na umaarufu wetu kwa sasa maisha yetu ni yakusubiri kufuturishwa tu.
Dude anasema kuwa wasanii kwa kukosa umoja wa ukweli katika maisha yao wamejikuta wakiwa ni watu wakutumiwa na wanasiasa na watu wenye fedha zao jambo linalofanya hata wanapokutana nao katika mialiko mbalimbali kuishia kula chakula na kupewa pesa za vocha tu na kusahau shida zao muhimu kuepuka kuuza haki ya kazi zao.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako