Friday 9 August 2013

MADRID ILIVYOIBUTUA CHELSEA THE BLUEZ VIJANA WA JOSE MOURINHO



Timu ya Zamani ya kocha mwenye maneno mengi mdomoni Jose Morinho Real Madrid imefanikiwa kuwapa kichapo cha mbwa mwitu timu mpya ya kocha huyo Chelsea the Blues kwa goli 3-1
Kiungo Frank Lampard alicheza kwa mara ya kwanza majira haya ya joto, lakini alishindwa kumzuia Cristiano Ronaldo kuinyanyasa Chelsea katika mechi hiyo.



Kabla ya mechi hiyo na Real Madrid mjini Miami, kiungo huyo mkongwe alikosa mechi zote za kujiandaa na msimu za klabu, Stamford Bridge kutokana na kuwa majeruhi.
Lakini Lampard ameimarika na kuanza kazi tayari kwa mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu dhidi ya Hull City, Agosti 18 baada ya kumaliza dakika 45 za kwanza katika Fainali ya Mabingwa wa Kimataifa wa Guinness.
Katika mechi hiyo, mabao mawili ya Ronaldo na moja Marcelo, yalitosha kuitotesha timu ya Jose Mourinho 3-1 dhidi ya timu yake ya zamani ambayo kwa sasa inafundishwa na Carlo Ancelotii,Chelsea ilipata bao lake pekee kupitia kwa Ramires.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako