Tuesday 6 August 2013

RONALDO AIKACHA MANCHESTER UNITED NA KUSAINI MKATABA MPYA REAL MADRID


LILE sakata linalomuhusu winga machachari zaidi Duniani Christian Ronaldo limepatiwa ufumbuzi mara baada ya mchezajii huyo kusaini mkataba mpya wa miaka mitano wenye thaman ya euro million 75.




Kwa kufanya hivyo Ronaldo atakuwa amekata mzizi wa tetesi zililizokuwa zikimuhusisha na kuhamia katika klabu yake ya zamani ya Manchestert United na kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika soka la Hispania akimpiku Lionel messi wa FC BARCELONA.
Gazeti la michezo la Madrid linalojulikana kwa jina la Marca linaripoti kuwa  Ronaldo atakuwa amempiga bao messi kwa zaidi ya paundi 900 millioni kwa mwaka ikilezwa kuwa Ronaldo ameongezewa umiliki wa haki za taswira yake alizokua akimiliki kwa asilimia 60,

Kwa kusaini mkataba mpya kutamfanya Ronaldo kumalizia maisha yake ya  soka akiwa na timu ya Real Madrid na kukata mzizi wa uvumi uliokuwa ukimuhusisha na kurudi katika klabu yake ya zamani Manchester united ya England.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako