Bingwa wa dunia wa kuruka kamba akionyesha medali
pamoja na kombe zawadi alizopata kwa ushindi huko Marekani.
Hamis Mohamed na wenzake wakionyesha umahiri wao wa
kuruka kamba ndani ya Ikulu jana jioni.
Rais Kikwete akitizama medali ambazo Hamis Mohamed
ameshinda kutokana na mchezo wa kuruka kamba.
Rais Kikwete akimpongeza Hamis Mohamed kwa kutwaa
ubingwa wa dunia na kuipa sifa Tanzania ambayo kwa miaka mingi haijashinda
medali yeyote katika michezo ya kimataifa.
Kijana Hamis Mohamed na wenzake jana jioni
walialikwa na Rais wa Tanzania, Rais Kikwete kupewa pongezi baada ya kushinda
ubingwa wa dunia katika mchezo wa kuruka kamba, mashindano yaliyofanyika hivi
karibuni Nchini Marekani.
Akimuelezea kijana Hamis Mwenyekiti wa Sport
Training Centre (TSTF), bwana Dennis Makoi amesema kuwa walipotambua kuwa
kijana huyo ana kipaji cha mchezo huo waliamua kumtafuta mfadhili ili
kukiendeleza kipaji chake. Aliongeza kuwa walipata mfadhili kutoka Marekani
ambaye anamiliki kituo cha kufundishia mchezo huo ambaye alimchukua Hamisi
kwenda Marekani Desemba mwaka jana kwa ajili ya kuendeleza mafunzo kwa kijana
huyo.
Makoi aliendelea kusema kijana huyo akiwa katika
kituo cha mfadhili huyo alishiriki mashindano ya dunia ya mchezo wa kuruka
kamba yaliyofanyika Julai 5 hadi 13 mwaka huu jijini Orlando, Marekani ambapo
yalishirikisha washiriki 480 kutoka timu 44 kwenye nchi 14 na Tanzania ilitoa
jumla ya wachezaji 6 akiwemo Hamis aliyeongoza na kunyakua kombe hilo.
Amy Canady ambaye ndiye alimchukua na kumfadhili
kijana Hamis alisema kuwa amefurahishwa na jitihada za kijana huyo ambapo
anafaa kuwa mfano na kupewa usimamizi mkubwa, pia amesema lengo lao ni kujenga
kituo cha mchezo huo Tanzania ili kuukuza ambapo vijana watapata fursa ya
kucheza wakiwa nchini kwao na kuitangaza vyema Tanzania.
Hamisi mwenyewe alisema anashukuru kwa malezi
aliyoyapata katika kituo cha watoto yatima cha Dogodogo Centre na kwa msaada
waliojitolea katika kuendeleza kipaji chake.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako