Jeshi la Polisi Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam, limetangaza dau la Sh100 milioni kwa mtu
atakayewezesha kupatikana kwa taarifa za kundi la uhalifu linalojihusisha na
vitendo vya kuwamwagia maji baadhi ya watu yanayodhaniwa ni tindikali.
Hatua hiyo inatokana
na vitendo hivyo kushamiri maeneo mbalimbali nchini.
Kamanda wa Polisi
Kanda hiyo, Suleiman Kova, alisema vitendo hivyo havipaswi kuvumiliwa na
kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa kuwafichua watu hao.
“Nimeamua kuomba
fedha hizi serikalini ili nimpe mtu atakayewezesha kupatikana kwa taarifa hizo,
hatimaye kukomesha vitendo hivi. Kemikali hii imekuwa na madhara makubwa,”
alisema Kova.
Hivi karibuni
Mkurungezi wa Maduka ya Home Shopping Center, Mfanyabiashara wa Lebonon na raia
wawili wa Uingereza walimwagiwa maji yanayodhaniwa ni tindikali.
Wakati huohuo, polisi
linamshikilia raia wa Uingereza kwa tuhuma za kukutwa na nyara mbalimbali za
Serikali zenye thamani ya zaidi ya Sh100 milioni, vikiwamo vipande vinane vya
meno ya tembo.
Kova alisema
mtuhumiwa huyo ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Usafirishaji Mizigo (TALL),
alikamatwa juzi saa 2:00 usiku maeneo ya Mbezi Beach, wilayani Kinondoni.
Alisema alipopekuliwa
nyumbani kwake alikutwa na meno 20 na kucha 22 za Simba, shanga mbalimbali
zilizotengenezwa kwa meno ya tembo, Kasuku na nyara nyingine ambazo hairuhusiwi
kumiliki bila kibali.
Alisema uzito wa
nyara hizo ni kilo 25, walimkuta na mawe mbalimbali yanayodhaniwa ni madini
sambamba na ganda moja la bomu lenye ukubwa mita 130.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako