Mchezaji wa Zamani wa Coastal Union ya
Tanga, Idrisa Ngulungu amefariki dunia mapema leo.
Idirisa Ngulungu alitamba sana na Timu
ya Coastal Union mwishoni mwa miaka ya 80 hadi mwishoni mwa miaka ya 90.
Alikuwepo kwenye kikosi kilichotwaa
ubingwa wa Tanzania bara mwaka 1988.
Kwa mujibu wa kaka wa Marehemu, Hussein
Ngulungu ambaye naye ni mchezaji wa zamani wa Taifa Stars amesema kuwa Idrisa
amefariki dunia kwa ajali ya gari iliyotokea eneo la Kisaki Mkoani Morogoro.
Hussein Ngulungu ameiambia PATAPICHA
kuwa Idrisa na ndugu wengine walikuwa wanaelekea Kisaki kwenye mazishi na kwa
bahati mbaya gari walilokuwa wanasafiria lilichomoka tairi la mbele na
kusababisha ajali hiyo iliyopoteza maisha ya Idrisa pamoja na ngudu yake
mwingine wa kike.
Akaongeza kuwa bado wanasubiri utaratibu
wa kupata mwili wa marehemu na baada ya kuupata utaratibu wa mazishi utafuata
ambapo mazishi yanategemea kufanyika kesho, Morogoro Mjini.
Inna lilah wainah lilah rajiun
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako