Thursday 15 August 2013

RAIS KIKWETE ALIPOKABIDHIWA JEZI YAKE IKULU

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bi. Kushilla Thomas akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete jezi iliyosainiwa na wachezaji wote wa timu ya FC Barcelona Ikulu jijini Dar es salaam ikiwa ni kutambua mchango wake katika kuendeleza soka na  ishara ya  ushirikiano wa kihistoria kati ya Castle Lager na FC Barcelona uliosainiwa hivi karibuni huko Camp Nou Hispania. Wanaotazama ni Meneja Mauzo wa TBL Kanda ya Kusini James Bokella (wa kwanza kulia) na Meneja Masoko wa TBL Bi. Natalia Celani (wa pili kulia). Na kushoto ni Meneja wa Castle Lager, Kabula Nshimo na Aggrey Marealle, Mkurugenzi wa Executive Solutions washauri wa mahusiano wa TBL.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako