'Human branding' ambayo inajulikana pia kama 'scarification',
ndo kitu kinachoongoza sasa hivi kwenye sanaa ya kujichora mwilini na
mwingereza mwenye tatoo nyingi kuliko wote hakutaka kuachwa nyuma na style hiyo
mpya.
Matthew Whelan,33, kutoka Birmingham hajajifunika mwili wake
kutoka kichwani hadi vidole vya miguuni tu na sanaa ya ngozi bali hadi
jicho lake moja jeupe kaliweka tatoo na kuwa jeusi. Hicho kifaa kilichotumika
kumchora tatoo kinatumia nguvu ya umeme kuunguza kwenye nyama na ndio
kifaa hicho hicho kinatumika na madaktari wa meno au surgeons kuunguza seli za
kansa.
Lest Westwood, mchora tatoo aliyemchora alisema "Huwa
inanukisha studio yote mwili wake unapoungua na kuna hatari pia ambazo
zinaambatana na kujichora tatoo hivi, mwili unaweza ukapata shock".
Bwana Whelan alikua na miaka 9 tu alipoanza kutamani sana tattoo
na tangia hapo alitumia masaa 300 kwenye kiti cha wachora tatoo na
alitumia zaidi ya euro 20,000 kujipamba mwili wake.
Designs zake zilitoka kwenye maumbo ya nyoka, ng'e(scorpions) na
binadamu wa kutisha (vampires) hadi jina la TV program anayoipenda
sana ‘The Jeremy Kyle Show’ alijichora tatoo ya kipindi hicho kwenye
kisogo chake.
Hapo hapo, Whelan ambaye
amebadilisha jina lake kisheria na kujiita 'His Royal Majesty Body Art, King of
Ink Land' alisema anapenda kujifikiria kuwa yeye ni kipande cha sanaa
kinachopumua na kuishi.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako