Monday 12 August 2013

FEZA KESSY ATOKA NDANI YA JUMBA LA BBA

Mshiriki aliyekuwa amebaki katika jumba la Big Brother Africa, Feza Kessy ametolewa usiku wa Jumapili katika mjengo huo baada ya wiki chache kutolewa kwa mshiriki wa Tanzania mwingine aitwaye Ammy Nando na kuiacha Tanzania ikiwa haina mshiriki mwingine aliyesalia katika Jumba jilo.
Feza amekaa ndani ya jumba hilo kwa muda wa siku 70 hadi kupata bahati ya kuingia ndani ya tano bora ametolewa usiku wa kuamkia leo kwa kuwa na idadi ndogo ya kura. 
 
Mwanadada huyo aliyekumbwa na Skendo kadha wa kadha ndani ya jumba hilo, ikiwemo kushiriki tendo la ndoa na mshiriki kutoka Botswana anayejulikana kwa jina la O’neal (Aliyetoka wiki iliyopita) pia alionekana akimuogesha mshiriki kutoka Zimbambwe anayejulikana kwa jina la Hakeem.
Pia Feza alifanikiwa kuvishwa pete ya uchumba ndani ya Jumba hilo na mshirki kutoka Botswana O’neal ikiwa ni ombi la kupewa nafasi ya kuolewa na mbotswana huyo ambaye pia ni mwanamuziki.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako