Sunday 11 August 2013

BAADHI YA PICHA ZA DIAMOND AKIREKODI VIDEO YAKE SOUTH AFRICA

Baada ya PATAPICHA kupata fununu za Video iliyokwenda kurekodiwa ndani ya Jiji la kifahari nchini Afrika Kusini, video ya wimbo uitwao "Tumetoka Mbali" wa Diamond Plantinum ambao unasemekana kamuimbia mke wake mtarajiwa Penniel Mwingila Maarufu kama DVJ Penny ambaye ni mfanyakazi wa DTV, picha za matukio ya video hiyo zimetufikia mikononi.
 Video hiyo imerekodiwa bila ya Mhusika kufahamu chochote kuhusiana na kutungiwa wimbo na Mpenzi wake (haya yanathibitishwa na mahojiano aliyofanya Mhariri wa PATAPICHA na mwanadada Penny Mwezi uliopita)
Hizi ni baadhi ya picha ambazo zimepatikana, zikionyesha matukio mbalimbali ya kurekodi Video hiyo 
 Moja kati ya Magari ya Kifahari (Ferrari) likiwa na Plate Number yenye jina lake Diamond Platnumz ambalo litaonekana akiendesha katika video hiyo mpya inayotarajiwa kutoka mwishoni mwa mwezi huu
Jina la Crew ya WASAFI halikukosa ndani ya Video hiyo hapo Gari ikibadilishwa plate Number na kuwekwa jina la wasafi kwa minajili ya kurekodi baadhi ya vipande vya video yake
Kuwa wa kwanza kuitizama video hiyo hapa hapa PATAPICHA

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako