Wednesday, 31 July 2013
BONDIA MTANZANIA AMCHAKAZA MTHAILAND.
BONDIA OMARI KLIMWERI AKITANGAZWA KUWA MSHINDI KATIKA PAMBANO HILO |
BONDIA Omar Kimweri anayefanya shughuli zake
nchini Australia amemchakaza Bondia wa Thailand anayejulikana kwa jina la Ekkalak
Saenchan katika raundi ya kwanza.
BONDIA OMARI KIMWERI AKIMTUPIA KOMBORA BONDIA WA KITHAILAND
BONDIA OMARI KIMWERI AKIMTUPIA KOMBORA BONDIA WA KITHAILAND |
KIMWERI AKIMVIZIA MTHAILAND AMPE MAKONDE MAZITO |
PATAPICHA INAMPONGEZA KWA KUWATOA WATANZANIA KIMASOMASO NA KUWATAKA WENGINE WAONGEZE JITIHADA
source superd blog
KITU CHA MWISHO WANACHOJIANDAA KUKIFANYA MAN UNITED KUMSAJILI FABREGAS
MANCHESTER UNITED WATAWEZA KUSAJIL;I KIUNGO HUYO AMBAYE KOCHA WA BARCA BADO ANATAKA KUENDELDEA KUFANYA NAE KJAZI NDANI YA TIMU HIYO. |
MANCHESTER UNITED wanajiandaa kuvunja rekodi ya usajili kwa klabu yao kumsajili Cesc Fabregas kutoka klabu ya FC BARCELONA.Habari kutoka katika gazeti la Daily Mail la Uingereza linasema kuwa Mabingwa hao wa ligi kuu ya Uingereza watatoa dau la paundi million 35 kama ofa ya mwisho kumnasa kiungo huyo.
KOCHA WA MAN UNITED ANAYEMMEZEA MATE KIUNGO FABREGAS WA BARCELONA |
Tayari Manchester wameshatuma dau la paundi millioni 26 na 30 kabla ya kukataliwa na mabingwa hao wa Hispania. Ingawa Barcelona wametangaza waziwazi kutomuuza Fabregas, haswa kutokana na kocha mpya wa timu hiyo aliyesema anataka kufanya kazi na Fabregas na hivyo hayuko tayari kuona anauzwa.
FABREGAS |
REKODI YA UNUNUZI WA WACHEZAJI KWA KLABU YA MAN UNITED
- Roy Keane kutoka Nottingham Forest, Paund 3.75m (July 1993)
- Andy Cole kutoka Newcastle, Paund 7m (January 1995)
- Jaap Stam kutoka PSV, Paund 10.75m (July 1998)
- Dwight Yorke kutoka Aston Villa, Paund 12.6m (August 1998)
- Ruud Van Nistelrooy kutoka PSV, Paund 19m (July 2001)
- Juan Sebastian Veron kutoka Lazio, Paund 28.1m (July 2001)
KAVUMBAGU AJIGAMBA KUWA KINARA WA USHINDANI WA NAMBA YANGA
KAVUMBAGU AKITAMBULISHWA SIKU YAKE ALIPOSAJILIWA NA YANGA |
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Didier Kavumbagu, raia wa
Burundi, amekiri kuwa kutakuwepo na ushindani wa namba msimu ujao wa l;igi
katika timu hiyo lakini akasema anajipanga kuhakikisha anakabiliana na hilo.
Didier Kavumbangu mchezaji wa Yanga
aliyesajiliwa toka timu ya Olympique kutoka Burundi akionekana haswa kutoka
katika michuano ya kombe la Kagame, Amesema atahakikisha anajifua kwa bidii
zaidi ali awe fiti na aweze kumshawishi kocha wa Yanga Brants aweze kumpanga
katika kikosi hicho cha mabingwa wa soka wa Ligi kuu ya Tanzania bara
“Ninakubali na najua
kuwa kutakuwa na ushindani mkubwa t “Nitajituma kwa nguvu zangu zote
kuhakikisha sipotezi nafasi yangu,” alisema Kavumbagu.faut naule wa msimu
uliopita lakini najitahidi kuhakikisha sipotezi nafasi yangu Alisema Kavumbagu.
KAVUMBAGUUUUUUUU |
Alisema
najuakusajiliwa kwa washambuliaji wengi kwenye timu yetu kumefanya kuwa na
changamoto na nitakuwa nashindania namba dhidi yao lakini najianmini na naamini
nitashinda katika hilo kwa maendeleo ya timu yangu.
MBEYA BABA AMBAKA MWANAWE NA KUMZALISHA
YUSSUF AMANI ALIYEHUKUMIWA KIFUNGO CHA JELA MIAKA 30 KWA KUMBAKA MTOTO WAKE WA DAMU |
MAHAKAMA ya mkoani Mbeya imehukumu kifungo cha kwenda jela
miaka 30 mkazi wa Isanga Bw Yusuf Aman baada ya kumtia hatiani kwa kosa la
kumlawiti na kumzalisha binti yake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 15( jina
linahifadhiwa).
NI AIBU SANA BWANA AMANI AKIJIZIBA SURA KUKWEPA CAMERA ZA WAANDISHI WA HABARI KUPATA SURA YAKE |
Mwendesha mashitaka
wa serikali Archiles Mulisa aliiambia mahakamani hiyo Mbele ya
Hakimu Gilbert Ndeuruo kuwa Mshtakiwa huyo BwYusufu Amani (39) anayedaiwa
kumbaka mwanaye wa kumzaa kisha kumzalisha baada ya kutengana na mkewe.
Alisema kosa hilo ni
kinyume cha sheria kifungu cha 154 (1)a na 155 sura ya 16 iliyofanyiwa
marekebisho mwaka 2002, pamoja na kifungu cha 158(a) cha makosa ya
kuzini.
akisoma Hukumu hiyo
Hakimu Ndeuruo alidai kuwa Mtuhumiwa alianza kujihusisha kimapenzi na mwanaye
Mwaka 2008 baada ya kutengana na mkewe ambapo Mtuhumiwa aliachiwa watoto wote.
Aliongeza kuwa wakati huo binti huyo alikuwa na umri wa
miaka 12 na alikuwa akisoma shule ya msingi darasa la Tano jambo ambalo
wamedumu nalo kwa Miaka mine hadi ilipogundulika kuwa binti alikuwa mjamzito
Mei, 2012.
Alisema mbinu aliyokuwa akiitumia ni kumtishia binti asitoe
taarifa kwa mtu yoyote na kwamba baada ya kugundulika kuwa na ujauzito
alimwambia amsingizie kijana yoyote mtaani kwao.
Hakimu Ndeuruo alisema Mahakama ilimtia hatiani Mtuhumiwa
kutokana na ushahidi wa Mhanga wa tukio hilo ambaye ni binti pamoja na ushahidi
wa kitaalamu kutoka kwa Mkemia mkuu wa Serikali.
KULIA NI MTOTO ALIYEZALISHWA NA BABAAKE AKIWA AMEBEBA MWANAWE HUYO |
Alisema ushahidi wa Mkemia Mkuu wa Serikali baada ya kupima
Vinasaba kutoka Mtuhumiwa, Mhanga na Mtoto aliyezaliwa ulidai kuwa Mshtakiwa ndiye baba halali wa Mtoto kutokana
na Maeneo 15 ya vipimo vya Vinasaba kati ya Baba na Mtoto aliyezaliwa kufungana
kwa asilimia 99.9.
Aidha kabla ya kutoa hukumu Hakimu alimpa nafasi mtuhumiwa
kujitetea ili apunguziwe adhabu au asiweze kuhukumiwa kabisa lakini hali ikawa
tofauti baada ya Mtuhumiwa kujibu kuwa hana la kujitetea vyovyote itakavyokuwa
anachotaka ni nakala ya hukumu.
Kutokana na kushindwa kujitetea Hakimu Ndeuruo alimhukumu
kwenda jela miaka 30 na kwamba ana haki ya kukata rufaa katika Mahakama kuu
endapo hakuridhika na hukumu hiyo.
Awali katika ushahidi wake Mahakamani hapo Mtuhumiwa huyo
alidai kuwa hakutenda kosa hilo bali alitengenezewa na Mkewe ambaye aliapa
kumkomesha baada ya kukosana na kumpata mume mwingine jambo ambalo lilipingwa
vikali na hakimu na kudai kuwa “ mfa maji haachi kutapatapa” Na kasha kutoa
hukumu hiyo
Subscribe to:
Posts (Atom)