Taarifa ambazo zimetufikia hivi
punde zinasema kuwa Askofu Mkuu wa Evangelistic Assemblies God Tanzania, Moses
Kulola amefariki dunia takriban dakika 25 zilizopita.
Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika
kutoka kwa watu wa ndani wa familia hiyo, zinaeleza kuwa Askofu Kulola
amefariki katika hospitali ya AMI (African Medical Investments) iliyopo Slipway
jijini Dar es Salaam.
Askofu Kulola, ambaye amezaliwa
mwaka 1928, amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na hata kufikia
hatua ya kupelekwa nchini India kwa matibabu.
Katika uhai wake, amepata watoto
wengi wa kiroho ikiwemo Dr Daniel Kulola, Mchungaji Florian Katunzi, Zakaria
Kakobe, Mzee wa Upako, Maboya, Mwasota na wengineo wengi.
BWANA ametoa na BWANA ametwaa, jina
la BWANA lihimidiwe.
HISTORIA YA ASKOFU MOSES KULOLA
Moses Kulola, alizaliwa mwezi Juni
1928, katika familia ya watoto kumi, na watano kati yao bado ni hai.
alisajiliwa katika shule ya kwanza mwaka 1939 iitwayo Ligsha Sukuma shule ya
misheni baada ya Ligsha, alijiunga na taasisi ya usanifu mwaka 1949. Alibatizwa
mwaka 1950 katika Kanisa la AIC Makongoro.
Ni mume wa Elizabeth na wamezaa
watoto10 ambapo saba bado hai.alianza kazi za kimisionari mwaka1950 japokuwa
aliitwa mwaka 1949 mara tu baada ya kubatizwa.
Mwaka
1959 alianza kufanya kazi serikalini, wakati huo huo akihubiri Injili katika
miji na vijiji. Utumishi wake mkubwa kwa nchi ulifika mwisho mwaka 1962, ambapo
aliamua kujitolea moja kwa moja nguvu zake zote, mwili na nafsi. Mwaka 1964
alijiunga na chuo cha kiteolojia na 1966 alitunukiwa stashahada.
Hakuacha elimu pale tu, aliendelea na masomo mbalimbali
ambapo alitunukiwa vyeti mbalimbali katika mataifa mbalimbali.
Alihudumu kikazi kwa miaka miwili
kama Mchungaji kabla ya kuwa mpentekoste mnamo 1961-1962, alifanya kazi katika
kanisa la TAG 1966 mpaka 1991 ambapo aliamua kuanzishaa makanisa Evangelistic
Assemblies God (EAGT), ambapo yalifanikiwa kukua kwa kasi kubwa katika nchi za
Tanzania, Zambia , Malawi na kwa ujumla kuna makanisa yapatayo 4000 katika nchi
mbalimbali yakiwemo makubwa na madogo Askofu Moses Kulola anayeongoza makanisa
elfu nne, Askofu Msaidizi wake ni Mwaisabila.
Askofu Kulola aliyeketi akiwa na waimbaji wa injili
nchini Mwinjilisti Faustin Munishi mkono wa kushoto pamoja na Emmanuel
Mwasota, mwanzoni mwa mwaka 1970
|
Mchakato wa kuongoza makanisa elfu nne si rahisi na
kwamba kumefanyika mgawanyiko wa majimbo yasiyopungua 34 ya kazi na kanda tano
kwa ajili ya kurahisisha kazi na kila kanda na jimbo lina mwangalizi wake.
Nampenda sana Askofu Moses Kulola maana anafanya kazi ya
MUNGU kwa moyo na kwa mujibu wa kitabu cha historia yake Askofu Kulola
amezunguka Tanzania nzima tena wakati mwingine kwa kutembea kwa miguu na kwenye
mazingira magumu sana kiasi kwamba ni wito mkuu wa MUNGU mkuu alionao Askofu
Kulola na kwa miaka zaidi ya 60 amekuwa akihubiri neno la MUNGU na hadi sasa
MUNGU anamtumia sana, katika mkutano uliopita wa askofu Kulola pale viwanja vya
jangwani jijini Dar es salaam maelfu ya watu walihudhulia na wengi sana
kufunguliwa na injili anayohubiri askofu Kulola ni injili iliyonyooka na
akiwataka wanadamu kumpa YESU KRISTO maisha yao ili wapate uzima wa milele
bure.
Ukiacha mengi ambayo Mungu
anaendelea kumtumia mtumishi wake huyu, kuna suala la nywele zake, askofu
Kulola kama tulivyowahi kuandika siku zilizopita, hajanyoa nywele zake kwa
takribani miaka 47 sasa, kwakuwa hakupendezwa na suala la kwenda salon kunyoa
nywele zake hivyo akamwambia Mungu nywele alizokuwa nazo kwa wakati huo zisikue
zaidi au kupungua, na ndivyo ilivyo mpaka sasa wembe haujapita kichwani mwake.