HABARI
zilizotufikia hivi punde kutoka katika mtandao mmoja wa kimichezo nchini
umemnukuu mmoja wa watu wa karibu wa klabu ya soka ya Dar es salaam Young
Africans akithibitisha kuwa klabu hiyo haitashiriki michuano ya kagame
itakayoandaliwa katika jimbo la Darfur nchini SUDAN.
Hatua hiyo
imekuja kufuatia tamko la waziri
anayehusika na mambo ya nje nchini Mh Bernard Membe aliyotangaza bungeni
kuwa jimbo la Darfur linalotarajiwa kuwa miongoni mwa sehemu zitakazochezwa
michuano hiyo hazina usalama, na wageni wanaofika huko huvishawa flana
zinazozuia risasi(Bullet proof) kwa ajili ya usalama wao.
Pia Waziri huyo alitanabaisha kutokuwepo kwa
hoteli zenye hadhi ya kupokea wageni na kuzishangaa timu zinazojiandaa kuelekea
huko.
Tayari
vilabu vikubwa vyenye ushawishi katika ligi hiyo vimeshatangaza kutopeleka
timu katika jimbo hilo DARFUR SIMBA YA
TANZANIA, TUSKER YA KENYA,AL HILAL NA
EL- MEREIKH ZOTE ZA SUDAN KUSIN,
Mashindano
ya kagame huandaliwa kila mwaka yakijumuisha vilabu bingwa vya ukanda wa Afrika
mashariki na kati na Dar es salaam Young Africans ndio mabingwa watetezi wa
kombe hilo.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako